KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb
UKURASA; 77 – 86

Kila mtu pale alipo, ana fikra ambazo zinatawala akili yake na pia zinatengeneza imani yake.
Kile unachoamini sasa hakikutoka tu hewani, bali kiliingia kwa njia mbalimbali.

Vipo vyanzo vikuu vitatu ya taarifa na maarifa yanayojenga fikra na imani.
1. Njia za mawasiliano, hapa kuna vitabu, cyombo vya habari, mtandao wa intaneti.
2. Watu, ambapo kuna familia, walimu, viongozi wa dini, viongozi wa kisiasa n.k
3. Uzoefu wako binafsi, hapa unatengeneza imani kulingana na yale uliyopitia.

Matangazo mbalimbali ya kibiashara yamekuwa yanatengenezwa kwa njia ambayo yanabadili kabisa imani ambazo watu wanazo.
Katika kujijengea kufikiri kwa kina na kuwa na imani sahihi, lazima uhoji kila unachofikiri na kuamini, ujue kimetoka wapi na pia uhoji usahihi wake.

Hii ndiyo ilimwezesha Leonardo kuweza kufanya makubwa, kwa sababu hakukubali mambo kirahisi. Badala yake alikwenda ndani zaidi na kuweza kuujua ukweli.
Leonardo da Vinci anasema kwamba uongo mkubwa ambao unawatesa watu ni maoni yao binafsi. Ukishakuwa na maoni na ukafikiri hayo ndiyo sahihi kuliko mengine, hapo ndipo unapoanza kujidanganya.

Tuwe makini na vyanzo vya maarifa, taarifa na imani zetu. Tuhoji ili kujua ukweli.

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa