To understand the true quality of people, you must look into their minds, and examine their pursuits and aversions. – Marcus Aurelius
Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya nakubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari NJIA YA KUWAJUA WATU VIZURI…
Watu wanaweza kutuhadaa kwa mwonekano wao, kwa mavazi, kile wanachofanya na hata tabia wanazoonesha katika maeneo fulani.
Lakini ipo njia moja ambayo ni vigumu mtu kukuhadaa.
Kuna njia ambayo mtu kamwe hawezi kuficha kile ambacho kipo ndani yake.
Na njia hiyo ni FIKRA ambazo mtu anazo.
Ukitaka kumjua mtu vizuri, angalia fikra zake.
Angalia ana mawazo gani juu ya kile unachoangalia.
Angalia ni mtazamo upi ambao anao kwenye kile unachoangalia.
Na kwa hakika utampata mtu, jinsi alivyo, bila ya kificho.
Mawazo na fikra zetu zipo wazi kwa kila mtu, hivyo tunapaswa kuhakikisha mawazo yetu ni bora kabisa wakati wote. Tunahitaji kuwa na fikra sahihi kwa kile tunachofanya.
Nakutakia siku bora sana ya leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa