KITABU ; Meditations / Marcus Aurelius.
UKURASA; 29 – 38.

Muda wa maisha yetu hapa duniani ni mfupi sana.
Muda huu una ukomo, hivyo chochote ambacho mtu unapanga kufanya, ni vyema ukakifanya kwa muda ulionao sasa.
Kuahirisha mambo na uvivu mwingine wowote wa kusema nitafanya, ni kujaribu kupoteza muda huu wa thamani tulionao.

Hitimisho la maisha yetu wote hapa duniani ni kifo. Hakuna mtu anayeweza kukiepuka kifo. Kifo ni njia ya asili ya kila kiumbe hai. Hivyo mtu yeyote anayehofia kifo, ni mtoto. Njia pekee ya kunufaika na kifo, ni kufanya kile unachofanya kwa wakati unaopanga kufanya.

Chochote ambacho tunakutana nacho kwenye maisha hakidumu. Iwe ni umaarufu au aibu, iwe ni kupata au kukosa. Lakini kitu pekee ambacho ni muhimu kwenye maisha yetu ni kuishi falfasa.
Kuchagua falsafa ambayo inaendana na sheria za asili na kisha kuishi falsafa hiyo.
Falsafa ndiyo inatupa mwongozo wa namna ya kuishi vyema leo ili kuweza kukabiliana na lolote tunaloweza kukutana nalo wakati wowote.

Ishi sasa, kwa kufanya kile ulichopanga kufanya, jua kifo ni sehemu ya maisha na usikihofie na ishi falsafa inayoendana na sheria za asili.

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa