For greed all nature is too little. – Lucius Annaeus Seneca

Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio?
Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari TAMAA HAISHIBI…
Tamaa ni mtego mbaya sana,
Ni shimo refu ambalo ukianza kulichimba hufiki ukingoni,
Ni tumbo ambayo haishibi chochote.
Tamaa huzaa tamaa zaidi,
Mtu anaweza kutamani kitu fulani, akishakipata anagundua kuna vingine bora zaidi, na hivyo anakuwa na tamaa zaidi.

Kwa njia hii mtu hafurahii wala kuthamini kile alichopata, badala yake anakazana na kile kipya anachotamani.
Hii inapelekea mtu kukosa shukrani na kuishi maisha ya kukimbiza vitu maisha yake yote.

Ili kuyafurahia maisha, ili kuona maana ya maisha yako, dhibiti tamaa zako. Jali kila unachopata, shukuru kwa kila jambo na wakati wowote, kuwa huru kwa chochote. Usijiambie maisha yako hayajakamilika mpaka upate vitu fulani. Maisha yako yamekamilika hapo ulipo sasa. Ishi maisha yako na ridhika nayo, huku ukiendeleankuwa bora zaidi.

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha