Huwa tunapenda kufurahia michezo mbalimbali, ambapo wachezaji wanacheza na sisi tunaburudika.

Lakini katika kila mchezo, watu wanaumia. Iwe ni mchezo wa ngumi, wachezaji wanapigana na wanaumia. Hata mchezo wa mpira wa miguu au mikono, wachezaji wamekuwa wanaumia uwanjani.

wp-image--1475273682

Pamoja na maumivu hayo, wachezaji hawaachi kucheza. Watauguza majeraha na kurudi tena uwanjani kutoa burudani kwa wengine.

Sasa hilo tukiliona kwa wachezaji tunaona ni kawaida, ila linapotokea kwenye maisha yetu tunaona tunaonewa au siyo sawa kwetu.

Ukweli ni kwamba maisha ni mchezo na maumivu ni sehemu ya huu mchezo. Kila mtu ana eneo lake katika mchezo huu, na kila eneo lina maumivu yake. Kadiri unavyochukua hatua unakutana na maumivu, na kadiri hatua unazochukua zinavyokuwa kubwa, ndivyo maumivu yanavyokuwa makali.

SOMA; UKURASA WA 138; Nguvu Haipo Nje, Nguvu Unayo Ndani Yako…

Ninachotaka kukukumbusha rafiki yangu ni hichi, usikimbie wala kulalamikia maumivu, maumivu ni sehemu ya mchezo huu wa maisha.

Hivyo kwa hatua unazochukua na kukutana na maumivu, jiulize ni kipi unapaswa kujifunza hapo, ni hatua zipi unapaswa kuchukua ili kuweza kupiga hatua zaidi.

Unapokutana na maumivu furahia kwa sababu maumivu yanakukomaza, pia jua umefanya kitu ambacho hujazoea kufanya na hivyo unakua zaidi.

Maumivu yanakufanya kuwa imara zaidi, yanakufanya ujue nguvu iliyopo ndani yako ambayo hujawahi kuijua.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog