Kwenye zama hizi za taarifa, ambapo mitandao ya kijamii imekuwa na nguvu kubwa kwenye maisha yetu, kitu kinachoumia sana kwenye maisha ya wengi ni utu, ile hali ya kujithamini kama mtu, ambayo inaanzia ndani ya mtu mwenyewe.

Hali hii inaumia kwa sababu watu hawawezi tena kujithamini wenyewe, bali kusubiri mpaka wengine wawathamini. Mpaka aweke picha kwenye mitandao ya kijamii na watu waipende na kumsifia kwamba amependeza, yupo vizuri na kadhalika.

Mitandao

Hali hii ndiyo naiita kukodisha utu wako kwa wengine na ni hali inayowaumiza wengi pamoja na kupelekea watu kutokujiamini. Mtu hawezi kujiamini yeye mwenyewe kwamba anaweza au yuko vizuri, mpaka pale wengine watakapomwambia hivyo.

Sasa changamoto kubwa sana kwenye hili ni kwamba, kila mtu anakazana kutaka kuonekana na wengine, hivyo hakuna hata anayeangalia. Yaani wakati unakazana kufanya mambo ili watu wakuone na kukuthamini, na wao wanakazana kufanya ili waonekane na wathaminiwe.

SOMA; UKURASA WA 780; Hakuna Wa Kukuzuia Tena…

Hivyo kila mtu anakazana aonekane na watu ambao hata hawaangalii. Na hili ndiyo linafanya mambo kuwa magumu na mabaya zaidi.

Usikodishe utu wako kwa wengine, usisubiri mpaka wengine wakuthamini ndiyo ujithamini. Wewe ulivyo umekamilika na una kila unachohitaji kuweza kuendesha maisha yako, jikubali na jithamini na hili litakuwezesha kuchukua hatua muhimu kwenye maisha yako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog