Whatever the universal nature assigns to any man at any time is for the good of that man at that time. – Marcus Aurelius

Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio?
Ni nafasi nyingine nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA tuna uhakika wa kufanya makubwa.
Na kwa mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA mwaka huu 2018 utakuwa mwaka wa kupiga hatua kubwa zaidi.

Asubuhi ya leo tutafakari ULICHONACHO NDIYO KINAKUFAA KWA SASA…
Kila mtu anapenda kupiga hatua zaidi kwenye maisha yake,
Kila mtu anapenda kufanikiwa zaidi kwenye maisha,
Na kila mtu anapenda kuwa juu zaidi kimaisha.
Lakini siyo wote wanaoweza kuanzia juu, na hivyo wengi wanaanzia chini, chini kabisa ambapo huwezi kupalinganisha na kule mtu anataka kufika.

Ni tabia ya wengi kudharau pale chini wanapoanzia na kuona siyo sahihi kwao. Hukazana kufikiria mbali zaidi na kukataa pale walipo sasa.
Na kwa kufanya hivyo, wanajikuta wanaendelea kubaki pale walipo.

Iko hivi rafiki, popote pale unapoanzia, hapo ndipo unapopaswa kuanzia.
Popote pale ambapo upo kwa sasa, hapo ndipo unapostahili kuwepo.
Kama unataka kupiga hatua zaidi, lazima uanzie hapo ulipo sasa.
Hivyo kupakataa na kuona hapakufai, kunakuzuia wewe kuweza kuchukua hatua sahihi.

Kubali pale ulipo sasa, hata kama siyo unapopapenda, kisha patumie kupiga hatua zaidi.
Ukipakataa utaendelea kubaki hapo kwa sababu hutaweza kupiga hatua zaidi.

Uwe na siku njema sana leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha