Nilishakushirikisha jinsi ya kusikiliza, leo nakwenda kukushirikisha jinsi ya kuongea.

Unaweza kushangaa kwamba kuongea nako inapaswa kujifunza? Si unatoa tu maneno uliyonayo?

Ni sababu hiyo ndiyo inapelekea wengi kuingia kwenye matatizo, kuongea kwa sababu tu wanaweza kuongea.

Mvuvi

Sasa tujifunze jinsi ya kuongea.

Ongea kwa sababu una kitu MUHIMU cha kuongea, na siyo kwa sababu tu unataka na wewe uongee.

Ongea kwa ufupi na kwa kueleweka, ukimaliza nyamaza.

Ongea kwa kueleza kile unachotaka mtu aelewe, kwa lugha rahisi kueleweka, kwa kuepuka maneno magumu au yenye maana tata.

Fikiria kwa kina kabla ya kuongea, ukijua baada ya kuongea huna tena nafasi ya kurudisha maneno uliyotoa.

Kila neno unalotamka, jua linasikilizwa na kila mtu, na siyo leo tu, hata miaka 50 ijayo, watu watalisikia.

Kadiri unavyoongea sana, ndivyo unajiweka kwenye nafasi kubwa ya kuongea kitu cha kijinga.

Kama kuna nafasi ya kuonesha, basi usiongee, onesha, fanya, matendo yana nguvu kuliko maneno matupu.

Jifunze jinsi ya kuongea kila wakati, maana maneno yamewaingiza wengi kwenye matatizo makubwa. Kuongea ni bure, lakini baada ya kuongea unaweza kulipa gharama kubwa sana.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog