“Men are born to succeed, not fail.” —Henry David Thoreau

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari UMEZALIWA KUSHINDA…
Kila unapoamka asubuhi,
Kila unapoweka malengo na mipango yoyote ya maisha yako,
Kila unapoanza kufanya chochote kikubwa,
Jikumbushe kauli hii muhimi; UMEZALIWA KUSHINDA NA SIYO KUSHINDWA.

Upo hapa duniani kwa ajilo ya ushindi,
Uwepo wako tu ni alama ya ushindi,
Kuwa kwako hai mpaka leo ni ushindi mkubwa sana.
Na chochote unachotaka kufanya, utakachopata ni ushindi.

Lakini wengi wamekuwa hawapati ushindi waliozaliwa kuupata, kwa sababu wamefundishwa kushindwa.
Wengi wamekubaliana na kushindwa, na kuona hayo ndiyo maisha yao.
Wanapokutana na ugumu au changamoto kidogo, basi wanatangaza kushindwa.

Umezaliwa kushinda, na huwezi kabisa kushindwa kama wewe mwenyewe hujachagua kushindwa.
Ishi kwa ushindi leo na ishi kwa ushindi kila siku, maana hayo ndiyo maisha halisi kwako.

Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya ushindi mkubwa kwako.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha