“Life consists of what a man is thinking of all day.” — Ralph Waldo Emerson
Hongera Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari NI KILE UNACHOFIKIRI MUDA WOTE…
Kitu kikubwa sana unachopaswa kukilinda muda wote kwenye maisha yako ni FIKRA ZAKO.
Kwa sababu maisha yako ni matokeo ya fikra zako.
Unakuwa kile unachofikiri muda wote.
Kama unakuwa na fikra hasi, fikra za kushindwa na fikra za mambo kuwa magumu, hivyo ndivyo maisha yako yatakavyokuwa.
Kama utakuwa na fikra chanya, fikra za ushindi na fikra za mambo kuwezekana, hicho ndiyo unapata kwenye maisha yetu.
Hakuna kinachotokea kwenye maisha yetu kwa bahati nzuri au mbaya. Kila kinachotokea kwenye maisha yetu ni zao la fikra zetu.
Chunga sana kila unachoruhusu kiingie kwenye fikra zako,
Chuja sana ni aina gani ya mawazo unaruhusu yatawale akili yako.
Kama kitu ni hasi, hakipaswi kupata nafasi kwenye akili yako.
Uwe na siku bora sana ya leo rafiki, siku ya kufikiri yale yaliyo sahihi ili uweze kuyapata.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha