Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari TABIA YA KUJIFICHA…
Moja ya kikwazo kikubwa kwenye mafanikio yako, ni tabia ya kujiicha.
Hii ni tabia ambayo kila mtu anayo, ila wanaofanikiwa wanaijua na wanaishinda.
Wale wasiofanikiwa, hawajui kama wana tabia ya kujificha, na ukiwaambia wana tabia ya kujificha, watakataa na hata kukuchukia kabisa.
Tabia ya kujificha ni pale unapokuwa na sababu kwa nini huwezi kufanya kitu fulani ambacho unajua ni muhimu kwako ili ufanikiwe.
Unajua kabisa ili utoke hapo ulipo sasa, unahitaji kufanya kazi kwa muda wa ziada na kuachana na mambo mengi yasiyo muhimu.
Lakini unaanza kujiambia kwamba huwezi kufanya hivyo kwa sasa, kwa kuwa bado hujajiandaa, au bado hujawa tayari au sababu nyingine yoyote.
Ukishaona tu una sababu kwa nini huchukui hatua sasa, jua unachofanya ni kujificha.
Kwa sabau chochote ambacho ni muhimu, unapaswa kukifanya sasa, na usisubiri kabisa kwa kutumia sababu yoyote.
Umepanga kuamka asubuhi na mapema, muda wakuamka umefika, ila unaanza kujiambia acha ulale kidogo, maana hata hivyo ulichoka sana jana, jua hapo unajificha.
Umepanga kuwasiliana na wateja wako, muda wakuwasiliana nao unafika, ila unajiambia siyo muda mzuri, labda watakuwa kweye kazi au hawatakuwa na muda wa kukusikiliza, jua hapo unajificha.
Unapanga kuanza biashara, lakini kila siku unasema huna mtaji, jua hapo unajificha.
Rafiki, nikukumbushe, kama kuna kitu muhimu sana unachohitaji kufanya, au ulichopanga kufanya, halafu wakati wa kufanya unakuja na sababu kwa nini usifanye, jua hapo unataka kujificha.
Wale wanaofanikiwa sana wanajikamata wenyewe kwa kujua sababu yoyote wanayotumia ni kujificha, na hivyo wanaanza kufanya.
Lakini wanaoshindwa hawajui kama ni kujificha, badala yake watasema na kujisidia mbele za watu, wakiamini sababu zao ni za msingi.
Hakuna sababu ya msingi kwenye kushindwa kufanya kile ambacho ni muhimu sana kwako kufanya.
Ukawe na siku bora sana leo, siku ya kuacha kujificha, siku ya kujitokeza na kufanya.
#Fanya AchaKujificha #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha