Wakati mzuri kabisa wa kumuuzia mteja mgumu kununua kwako, ni baada ya kuwa umekamilisha mauzo na mteja mwingine.
Unapokuwa umekamilisha mauzo unakuwa na hali ya kujiamini na unakuwa na ushawishi mkubwa sana.
Hivyo kama una mteja ambaye ni mgumu kununua kwako, anza kuwauzia wateja ambao ni rahisi kununua kwako, kisha ndiyo umuuzie mteja mgumu.
Lakini kama utaanza na mteja mgumu, ukishindwa kumuuzia utashindwa hata kuwauzia wateja ambao ni rahisi kununua kwako.
Wateja wote wa biashara yako hawafanani, wapo ambao wameshawishika na wapo tayari kununua kwako. Ila pia wapo ambao hawajashawishika hivyo unahitaji kufanya kazi kubwa ya ushawishi.
Anza kuwauzia walioshawishika kabla ya kuwauzia wanaohitaji ushawishi zaidi.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,