Unapotaka kujifunza zaidi kuhusu biashara, unahitaji kuziangalia biashara ambazo ni kubwa kuliko biashara unayoendesha wewe.

Hii ni kwa sababu biashara kubwa zina changamoto za tofauti na biashara ambazo siyo kubwa.

Na makosa wanayofanya wafanyabiashara wengi wanaoanza na biashara ndogo, ni kuendelea kuziendesha vile vile hata baada ya biashara kuwa zimeshakua zaidi.

Kadiri biashara inavyokua, changamoto zake zinabadilika na hivyo njia ya kuziendesha inapaswa kubadilika pia.

Sasa hutajua hilo kama hujifunzi kupitia biashara ambazo ni kubwa kuliko unayofanya wewe.

Chagua makampuni makubwa na yenye mafanikio kisha jifunze yanaendeshwaje. Angalia nini kimeyafikisha kwenye ukubwa yalipo sasa. Kisha tumia yale unayojifunza katika kukuza biashara yako zaidi.

Jifunze kupitia wale waliopiga hatua zaidi kuliko wewe na utaona wapi pa kuweka juhudi zaidi ili na wewe upige hatua zaidi.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha