Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KUFANYA NA KUTAKA KUONEKANA UNAFANYA…
Kwenye maisha, kuna makundi mawili ya watu.
Kuna watu wanafanya kitu kwa sababu wamechagua kufanya. Wanafanya kwa moyo wa kweli kwa lengo la kuleta matokeo ya tofauti kwao na kwa wale wanaowazunguka.
Watu hawa wapo tayari kwenda hatua ya ziada, wapo tayari kuteseka ili tu wapate kile wanachotaka.

Kwa upande wa pili, wapo wale ambao wanafanya kitu ili waonekane wanafanya. Kufanya kwao hakutoki ndani yao bali nje. Wanafanya pale watu wanapoangalia, lakini siyo kitu wanachoamini zaidi kwenye maisha yao.
Watu hawa hawapo tayari kuweka juhudi zaidi pale mambo yanapokuwa magumu.
Na huumia sana pale wale wanaotaka wawaone wakifanya hawajali sana.

Wanaofanikiwa kwenye maisha, ni wale wanaochagua kufanya kwa sababu wanajali na siyo kwa sababu wanataka kuonekana wanafanya.
Asubuhi ya leo tafakari kwenye kila unachofanya, kisha jiulize ndiyo unachojali kufanya kweli au unataka tu kuonekana unafanya.
Kama ndiyo unachojali hongera na endelea.
Kama unafanya ili uonekane, kumbuka maisha ni mafupim hivyo acha kuyapoteza kwa vitu visivyokuwa muhimu zaidi kwako.

Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kufanya kile unachojali zaidi.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha