“There are but two powers in the world, the sword and the mind. In the long run the sword is always beaten by the mind.” – Napoleon Bonaparte

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Tumepata nafasi nyingine nzuri na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari SILAHA KUBWA SANA UNAYOIMILIKI…
Napoleon Bonaparte, aliyekuwa mbabe wa kivita, anatuambia kuna silaha mbili kubwa duniani, UPANGA na AKILI.
Lakini mwisho wa siku, akili inaushinda upanga.

Anachotuambia ni kwamba, kila mmoja wetu, pale alipo, wnatembea na silaha kubwa sana, kubwa kuliko silaha nyingine zote hapa duniani.
Akilo yako ni silaha kubwa, unayoweza kuitumia kushinda chochote na kuweza kupata kile unachotaka, bila ya kujali ni ugumu kiasi gani umeupitia kwenye kupata unachotaka.

Akili zetu zina uwezo wa kuvuta chochote tunachotaka,
Akilo hizi zina uwezo wa kuwashawishi wengine wakubaliane na sisi,
Na pia zina uwezo mkubwa wa kuweka mipango dhabiti ya kufika kule tunakotaka kufika.
Na kwa hatari zaidi, akili zetu hizi zinaweza kuleta maangamizi makubwa sana kwetu na kwa wengine kama hatutaweaa kuzidhibiti vizuri.

Lakini pamoja na kila mmoja wetu kumiliki silaha hii kubwa, wengi sana hawajui uwezo mkubwa walioubeba, wengi wanatumia silaha hii kubwa kwa vitu vidogo vidogo na kushindwa kuitumia kwa vitu vikubwa.

Yaani ni sawa na mtu kwenda kununua kompyuta yenye uwezo mkubwa sana, na akalipia fedha nyingi, lakini akaja kutumia kompyuta hiyo kwa kazi moja tu ya kusikiliza muziki. Ataona ananufaika nayo, lakini hajui uwezo mwingine mkubwa sana wa kompyuta hiyo ambapo inaweza kufanya makubwa sana.

Hivi ndivyo ambavyo watu wengi wanatumia silaha yao kubwa, yenye uwezo wa kufanya makubwa. Wanaitumia kufanya yale waliyozoea kufanya, wakati wangeweza kuwa na ubunifu mkubwa. Wanaitumia kutengeneza hofu badala ya kutengeneza matumaini. Wanaitumia kufuatilia maisha ya wengine badala ya kufuatilia maisha yao binafsi.

Rafiki, asubuhi hii jitathmini ni kwa namna gani unatumia silaha kubwa kabisa unayoimiliki. Je unaitumia kwa mambo ya manufaa kwako au unaipoteza kwa vitu visivyo na msingi? Je unaidhibiti na kuizuia isilete madhara au unaiacha silaha hiyo ilete kila aina ya madhara?
Silaha ni yako, na mtu pekee wa kuitumia vizuri ni wewe.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kwenda kuitumia vizuri silaha yako kwa manufaa makubwa kwako na wale wanaokuzunguka.
#Fanya#HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Www.amkamtanzania.com/kocha