“We seldom learn the true want of what we have till it is discovered that we can have no more.” – Samuel Johnson
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari THAMANI YA KITU BAADA YA KUKIPOTEZA….
Sisi binadamu huwa tuna tabia ya kuzoea vitu ambavyo tunavyo,
Tunavizoea na kuona vitaendelea kuwepo muda wote,
Hivyo tunavichukulia poa na hatuvipi thamani kubwa.
Ni mpaka pale tunapopoteza vitu hivi ndiyo tunagundua thamani yake kwa uhakika.
Ni mpaka pale ambapo hatuwezi kuwa navyo tena, ndiyo tunakumbuka jinsi vilivyokuwa na umuhimu kwetu.
Hivyo rafiki, chochote ulichonacho sasa kwenye maisha yako, kinachochangia maisha yako kwenda vizuri, usikichukulie poa hata kidogo.
Jua kwamba kile ulichonacho hutaendelea kuwa nacho milele, hivyo kithamini na kukitumia vizuri wakati bado unavyo.
Vitu vyenye thamani kubwa sana kwenye maisha yetu huwa tunavichukulia poa sana, kwa sababu tunaviona kila siku.
Mfano afya zetu, zinapokuwa vizuri tunazichukulia kawaida sana, ni mpaka tunapokuwa na matatizo ya kiafya ndipo tunaona thamani halisi ya afya imara.
Kadhalika mahusiano yetu na wengine, kazi na biashara zetu, vipo vitu vingi tunavyochukulia kawaida, lakini wiku vinapoondoka ndiyo tunaumia hasa.
Rafiki, asubuhi hii tafakari umuhimu wa kilw ulichonacho kwenye maisha yako, jua thamani halisi ya kila ulichonacho na kipe uzito unaostahili.
Tumia vizuri kila ulichonacho na kwa wakati bado unacho.
Ukijua ya kwamba kuna siku hutakuwa nacho, hivyo kifaidi vizuri sasa.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuthamini kila kinachoendelea kwenye maisha yako na kutokuchukulia vitu kwa mazoea.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha