Hongera sana mwanamafanikio kwa nafasi nyingine nzuri sana tuliyoipata leo.
Ni fursa bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KAWAIDA INAUMIZA…
Kinachowatofautisha wale wenye maisha bora, yenye mafanikio na furaha, na wale ambao wana maisha ya hovyo, ya kushindwa na mateso, ni mtazamo ambao wanao kwenye chochote wanachofanya.
Wale wanaoshindwa, huwa wana mtazamo wa kufanya kwa kawaida kwenye chochote kile wanachofanya.
Hawataki kabisa kwenda hatua ya ziada wala kutoa thamani zaidi.
Hawataki kujiumiza hata kidogo ili kufanya kilicho bora.
Wao wanachofanya ni kile ambacho ni cha kawaida kabisa, kile kilichozoeleka.
Kama mtu ameajiriwa basi anafanya kile tu alichopangiwa kufanya na anakifanya kwa ukawaida sana, kwa kiwango cha chini sana kiasi kwamba hatafukuzwa.
Atahakikisha anaweka kiwango cha chini kabisa cha juhudi ambacho kitamfanya aonekane yupo, lakini siyo kumfanya aonekane wa tofauti.
Na kama malipo anayopata ni kidogo, basi anajiambia kabisa ndani yake kwamba ya nini ajisumbue wakati analipwa kidogo?
Rafiki, kawaida inaumiza sana,
Kuwa kawaida kunakuumiza kwa sababu unajua kabisa unaweza kufanya zaidi lakini hufanyi.
Kufanya chochote kwa ukawaida kunaumiza sana kwa sababu hakukutofautishi na yeyote na hivyo hakuna mchango mkubwa unaothaminiwa kutoka kwako.
Hatua ya kwanza na muhimu sana kuchukua kwenye maisha yako ni kukataa kuwa kawaida, kuepuka kabisa kufanya vitu kwa ukawaida.
Chochote unachojiruhusu kufanya, basi nenda hatua ya ziada, weka juhudi zaidi ili kuzalisha matokeo bora zaidi.
Kataa kabisa ukawaida.
Jamii zetu zinatukuza ukawaida, ukatae kabisa.
Kaa mbali na wale waliozoea kawaida, wanaokuona wewe ni wa ajabu kwa sababu hufanyi kwa kawaida.
Hawa ni watu walioshindwa na wanataka wanaowazunguka pia washindwe ili kushindwa kwao kusiwe aibu kwao.
Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki, siku ya kukataa kuwa kawaida ns kuacha kufanya kwa ukawaida. Kwa chochote utakachofanya leo, nenda hatua ya ziada, weka juhudi zaidi, fanya zaidi ya kawaida na utapata matokeo makubwa na ya tofautinna wengine.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha