“An achievement is a bondage. It obliges one to a higher achievement.” —Albert Camus

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari HATUA NDOGO KUELEKEA HATUA KUBWA…
Unawezaje kumla tembo?
Kwa kula kipande kimoja cha nyama na kuendelea na kipande kingine.
Hakuna mtu ambaye anaweza kumla tembo akiwa mzima mzima,
Ila kila mtu anaweza kula nyama ya tembo.

Kwa mafanikio yoyote makubwa unayotaka kufikia kwenye maisha yako, kwanza usibabaike na ukubwa wake.
Usiangalie mipango mikubwa uliyonayo na ukaanza kuwa na wasiwasi kama utaweza kuifikia.

Badala yake gawa mipango yote mikubwa uliyonayo kwenye hatua ndogo ndogo, ambazo unaweza kuchukua.
Gawa kwenye hatua ndogo kabisa ambazo hazitakushinda kuchukua, kisha anza kuchukua hatua.

Weka akili na nguvu zako zote kwenye hatua unayochukua kwa wakati unaochukua hatua, ukikamilisha hamia kwenye hatua inayofuata.
Kwa kufanya hivi, siku moja utastuka na kujikuta upo kwenye kilele cha mafanikio.

Hakuna anayeshindwa hili,
Hakuna lengo ambalo haliwezi kuvunjwa kwenye hatua ndogo ndogo za kuchukua kila siku.
Kama kweli unataka kupiga hatua kubwa unayotaka kwenye maisha yako, lazima uwe tayari kugawa malengo yako makubwa kwenye hatua ndogo ndogo na uwe na nidhamu ya kufanyia kazi kila siku.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki, siku ya kupiga hatua ndogo ndogo za kukusogeza karibu zaidi na mafanikio makubwa unayotaka kupata kwenye maisha yako.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha