“When I have a little money, I buy books; and if I have any left, I buy food and clothes.” — Erasmus of Rotterdam

Ni siku mpya,
Siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari NUNUA KWANZA KISICHOHARIBIKA…
Unapopata fedha, kipaumbele chako cha kwanza kinapaswa kuiweka fedha hiyo kwenye vitu visivyoharibika.
Hivyo kuiwekeza fedha hiyo kwa namna ambayo itakulipa zaidi baadaye ni kipaumbele muhimu.
Na moja ya njia za kuwekeza kila kipato unachoingiza ni kununua maarifa.
Kila unachojifunza ambacho kinakuwezesha kupiga hatua zaidi, hakiozi.
Kila unachojifunza kinakaa na wewe milele.
Watu wanaweza kukuibia, kukutapeli na hata kukudhulumu chochote ulichonacho, lakini hakuna wa kuweza kuyaondoa maarifa yaliyopo ndani yako.

Badala ya kukimbilia kununua vyakula na mavazi, ukitegemea kinachobaki ndiyo ununue maarifa, nunua kwanza maarifa na kinachobaki ndiyo ununue vyakula na mavazi.
Vyakula na mavazi ni vitu vinavyoharibika haraka, lakini maarifa utakayonunua yatakaa na wewe milele, hasa kama utayafanyia kazi.

Usiseme umekosa maarifa au huna fedha ya kununua maarifa. Kama unakula kila siku na kuvaa nguo kila siku, tatizo kwako ni namna ulivyoweka vipaumbele vyako.
Weka vipaumbele vyako sawa na utaweza kuwa na maisha bora sana kwako.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuweka kipaumbele kwenye upataji wa maarifa, kwa kuwekeza kwanza kwenhe vitu visivyoharibika.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha