Ni kile ambacho umepanga kufanya, kile ambacho ni muhimu zaidi kwa wakati huo.

Unapaswa kuweka akili yako yote na nguvu zako zote kwenye kitu kimoja ambacho umechagua kufanya.

Kugawa akili yako na nguvu zako kwenye mambo mengi kwa wakati mmoja ni kupunguza ufanisi wake.

Chukua mfano wa jua, jua likitawanywa kwenye dunia nzima linatoa mwanga na joto la kawaida. Lakini jua hili hilo likikusanywa sehemu moja kwa kutumia lensi linatoa joto kali sana linaloweza kuwasha moto na kutoboa chochote.

Kusanya nguvu zako kwenye kile ulichochagua kufanya na utaweza kukifanya kwa ufanisi mkubwa sana.

Na kama unafanya kitu kimoja lakini mawazo yako yapo kwenye kitu kingine, acha kila unachofanya na jikumbushe vipaumbele ulivyonavyo. Ukishajua kipi ndiyo muhimu zaidi, fanya hicho na achana na vingine vyote.

Kama una vipaumbele viwili kwa wakati mmoja, huna kipaumbele.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha