“All you need are these: certainty of judgment in the present moment;
action for the common good in the present moment;
and an attitude of gratitude in the present moment for anything that comes your way.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 9.6

Hongera sana rafiki kwa nasafi hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni fursa ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa kulala mapema na kuamka mapema tunapata zawadi ya AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA.
Pia kwa kusimamia msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari MAKUBWA MATATU MUHIMU…
Rafiki, ili tuwe na maisha bora, tunahitaji kuweka nguvu na juhudi zetu kwenye maeneo matatu muhimu;
Moja; mtazamo tulionao
Mbili; matendo tunayofanya
Tatu; maamuzi tunayofanya.

Kama Marcus anavyotuambia, tunachohiyaji ni uhakika wa maamuzi kwenye wakati tulionao, kuchukua hatua za matendo mema kwa wakatu tulionao na mtazamo wa shukrani kwa wakati tulionao.

Wakati pekee tunaoweza kuudhibiti na kuutumia ni wakati tulionao, hivyo kama kwa wakati huu tulionao tutadhibiti mtazamo tulionao, tukafanya maamuzi sahihi na kuchukua hatua sahihi, tutaweza kufanya makubwa na kupata matokeo mazuri kwa wakati tulionao.

Ukawe na siku bora sana ya lep, siku ya kufanya maamuzi bora, kuchukua hatua sahihi na kuwa na mtazamo wa shukrani.
#MaamuziBora, #HatuaSahihi, #MtazamoWaShukrani

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha