“Let all your efforts be directed to something, let it keep that end in view. It’s not activity that disturbs people, but false conceptions of things that drive them mad.”
—SENECA, ON TRANQUILITY OF MIND, 12.5

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.

Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa sana.

Kwa msingi wetu wa wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari FAFANUA MAKUSUDI YAKO….

Chochote unachofanya, hatua yoyote unayochukua, usichukue tu kwa mazoea au kwa sababu inabidi ufanye.

Badala yake fanya kwa kuwa unajua nini unataka na unakwenda kupata mwishino. Kila hatua unayochukua unapaswa kuwa na kusudi kubwa unalotegemea mwishoni.

Kama ambavyo Seneca anatuambia kinachotusumbua siyo hatua tunazochukua, bali kuwa na dhana potofu kwenye kile unachofanya. Kwa maneno mengine kufanya bila ya kujua ni wapi kile unachofanya kinakufikisha.

Jua kule unakokwenda na kila hatua unayochukua iwe inakusaidia kufika kule unakokwenda.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuelewa makusudi yako na kuchukua hatua zinazokufikisha kwenye makusudi hayo.

Wako Rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,

Kocha Dr Makirita Amani,

http://www.amkamtanzania.com/kocha