Huwa tunafikiri ukishapata fedha ndiyo unakuwa huru.
Lakini wengi wanaokazana kupata fedha ili wawe huru, wanagundua kadiri wanavyopata fedha zaidi ndivyo wanavyokosa uhuru zaidi.
Hivyo fedha haileti uhuru, badala yake uhuru ndiyo unaleta fedha. Na hapa tunazungumzia ule uhuru wa kawaida wa maisha, na siyo uhuru wa fedha. Uhuru wa fedha ni kitu kingine.
Uhuru unaleta fedha, kadiri unavyokuwa huru, ndivyo unavyoweza kutengeneza fedha zaidi na hata kukua zaidi.
Ndiyo maana wale wote ambao wapo kwenye njia za kuingiza kipato ambazo hazina uhuru, huwa hawapati kipato kikubwa. Ukiangalia kwenye ajira, kwa kuwa mlipaji ni mmoja, uhuru unakosekana na siyo rahisi kuamua ulipwe kiasi gani.
Lakini mtu ambaye anamiliki biashara, ambayo ina wateja wengi, ana wigo mpana wa kuingiza kipato, hategemei sehemu moja, na hivyo anakuwa huru zaidi na kipato chake kinakuwa kikubwa zaidi.
Uhuru unaleta fedha, kazana kuwa huru zaidi na utaweza kutengeneza kipato zaidi.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,