Rafiki yangu mpendwa,

Nipende kuchukua nafasi hii kukushukuru kwa namna ambavyo tumeendelea kua pamoja kwa miaka yote ambayo nimekuwa natoa huduma hii ya mafunzo na hamasa kwa ajili ya kupiga hatua zaidi kwenye maisha yetu.

Kwa kipindi kirefu, miaka zaidi ya mitano sasa, msingi mkuu wa masomo haya umekuwa kupitia mtandao wa intaneti. Hivyo mafunzo haya mazuri yameweza kuwafikia watu wachache sana, wale ambao wanaweza kutumia mtandao wa intaneti.

Lakini naelewa kabisa kwamba wapo watu wengi sana wanaoyahitaji mafunzo haya na yanaweza kuwasaidia sana, lakini hawatumii mtandao wa intaneti. Na mara kwa mara watu wamekuwa wakinikumbusha kuhusu hili, lakini kutokana na majukumu ambayo nimekuwa nayo kwa siku za nyuma, sikuwa na namna bali kutumia njia ya intaneti pekee.

Kuanzia mwaka huu 2019, sehemu kubwa ya majukumu yaliyokuwa yanachukua muda wangu mwingi huko nyuma yamepungua, na sasa napata muda zaidi wa kuweka muda na nguvu kwenye kutoa mafunzo kwa wengi wenye uhitaji.

SAMSUNG CAMERA PICTURES
SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018

Hivyo leo nakupa taarifa ya wewe na wengine kupata mafunzo zaidi kutoka kwangu, kwa njia ambayo siyo ya mtandao. Na hapa nitaorodhesha njia mbalimbali na jinsi ya kuzitumia.

  1. Mafunzo kwa wanafunzi.

Kama una shule au chuo na unahitaji wanafunzi wako wapate mafunzo basi nipo tayari kuja kutoa mafunzo haya. Pia kama unafanya kazi kwenye shule au chuo na mna programu za mafunzo na unahitaji nije kufundisha tuwasiliane na nitatenga muda wa kufanya hivyo.

  1. Mafunzo kwa wafanyakazi.

Kama umeajiri wafanyakazi na ungependa wapate mafunzo kutoka kwangu, basi nipo tayari kutoa mafunzo hayo. Pia kama unafanya kazi kwenye kampuni au taasisi ambayo ina programu za mafunzo na ungependa myapate mafunzo yangu, tuwasiliane na nitaweza kuwashirikisha mafunzo haya.

  1. Mafunzo kwa vikundi.

Kama mna kikundi cha aina yoyote ile na mngependa kupata mafunzo ya kupiga hatua na ya hamasa, nipo tayari kuwapa mafunzo hayo. Kikundi kinaweza kuwa VICOBA, kikundi cha maendeleo, kikundi cha kiukoo au kifamilia. Tuwasiliane kwa ajili ya kupata mafunzo hayo.

  1. Mafunzo kwa umma.

Kama una kituo cha redio au televisheni au kama una kipindi kwenye redio au televisheni na ungependa mafunzo yangu yawafikie wasikilizaji na watazamaji wako, basi nipo tayari kushirikiana na wewe kutoa mafunzo hayo. Tuwasiliane pale unapokuwa na uhitaji huo.

  1. Mafunzo ya semina.

Kama unaandaa semina mbalimbali na ungependa niwe mwezeshaji katika semina hizo, basi nipo tayari kushiriki kwenye semina hizo. Tuwasiliane pale unapokuwa na uhitaji huo.

  1. Makala za mafunzo.

Kama una gazeti au mtandao unaotoa mafunzo kwa watu, au kama wewe ni mwandishi au mhariri wa chombo cha habari na ungependa kupata makala za mafunzo kutoka kwangu, basi tuwasiliane na nitakuwa tayari kutoa mafunzo hayo.

  1. Aina nyingine ya mafunzo.

Kama kuna aina nyingine ya mafunzo tofauti na niliyotaja hapo, ambayo unafikiri naweza kutoa kwako au kwa watu wengine basi usisite kunijulisha, tutaona jinsi ya kukamilisha hilo na watu wakajifunza.

UTARATIBU WA NAFASI YA KUPATA MAFUNZO.

Kama umechagua niweze kutoa mafunzo kwa njia ambazo nimeshirikisha hapo juu, basi hapa kuna mambo muhimu ya kuzingatia.

  1. Kuhusu gharama.

Hakutakuwa na gharama yoyote ya ziada nitakayotoza kwa mwaka huu 2019, mafunzo haya nitayatoa bure kabisa. Lakini kama una utaratibu wa kulipa kwa mafunzo ya aina hiyo, nitapokea kile kiasi ambacho mmeweka kwa utaratibu huo. Na hasa hapa ni kwa upande wa semina na mafunzo kwa wafanyakazi au vikundi.

  1. Kama mafunzo yatafanyika mkoani.

Makazi yangu na shughuli zangu nafanyia jijini Dar es salaam, kama utahitaji nije kufanya mafunzo mikoani basi utagharamia nauli na malazi. Na kwa sababu ya uhaba wa muda, kama mkoa uko mbali na Dar es salaam, sehemu ambayo inahitaji usafiri wa siku nzima basi utapaswa kugharamia nauli ya ndege ili kuokoa muda wa kuja na kurudi.

  1. Muda wa kutoa taarifa.

Kwa sababu nafasi hii itachukuliwa na wengi, unapaswa kutoa taarifa mapema ili kuweza kupata nafasi ya mimi kutoa mafunzo. Na taarifa inapaswa kutolewa mwezi mmoja kabla ya tarehe ambayo unataka nitoe mafunzo. Kwa mfano kama mafunzo yako ni tarehe kumi mwezi wa tatu, basi taarifa inabidi niipate kabla ya tarehe kumi mwezi wa pili.

  1. Maeneo ambayo hayatahusisha nafasi hii.

Kuna baadhi ya maeneo ambayo hayatahusisha nafasi hii, na maeneo hayo ni kama ifuatavyo;

Moja; ushauri wa moja kwa moja, kama unataka tukutane kwa ajili ya ushauri wa moja kwa moja, basi utagharamia ada ya ushauri ambayo ni tsh 100,000/= (laki moja) ambayo unailipa kabla ya kuweka miadi ya kukutana kwa ajili ya ushauri. Tukishakutana kwa ajili ya ushauri, kwa mwezi mzima utakaofuata nitaendelea kukufuatilia kuhakikisha unatekeleza kile tulichoshauriana.

Mbili; semina ambazo watu wanalipia kushiriki. Kama unaendesha semina ambayo washiriki wanalipa ada, basi nafasi ya mimi kutoa mafunzo bure haitakuwepo. Badala yake tutajadiliana kiwango cha malipo kulingana na wingi wa watu na muda nitakaotoa mafunzo hayo.

Tatu; huduma za ukocha zitaendelea kama kawaida. Pia huduma nyingine kama za KISIMA CHA MAARIFA na programu mbalimbali za ukocha zitaendelea kama zilivyokuwa. Kujiunga na programu hizi utapaswa kulipa ada ambayo imewekwa.

Karibu sana rafiki yangu tufanye kazi pamoja kwa maendeleo yako binafsi na wale ambao unapenda niwashirikishe mafunzo haya. Kwa muda wote ambao nimekua natoa mafunzo haya kwa njia ya mtandao nimejifunza mengi kupitia mafunzo ninayopata na hata watu ninaowafundisha na kuwakochi, hivyo nina mengi ambayo naweza kushirikisha kikundi cha aina yoyote na kikanufaika sana.

Kupata maelezo zaidi na hata kutuma maombi ya kupata mafunzo kama nilivyoelekeza hapa, tumia mawasiliano yafuatayo;

Simu; +255 717 396 253 au +255 755 953 887

Barua pepe; maarifa@kisimachamaarifa.co.tz au amakirita@gmail.com

Karibu sana tushirikishane maarifa na hamasa ya kuchukua hatua zaidi ili tuweze kufanikiwa zaidi.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge