“Keep this thought at the ready at daybreak, and through the day and night—there is only one path to happiness, and that is in giving up all outside of your sphere of choice, regarding nothing else as your possession, surrendering all else to God and Fortune.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 4.4.39

Ni siku nyingine mpya kwetu rafiki,

Siku bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari NJIA YA KUELEKEA KWENYE UTULIVU…

Kuna kitu kimoja ambacho falsafa ya ustoa inakisisitiza sana, kitu ambacho tunaweza kusema ndiyo msingi muhimu wa falsafa hii na msingi wa maisha ya utulivu na furaha.

Kitu hicho ni kujua yaliyo ndani ya uwezo wako na yaliyo nje ya uwezo wako.

Njia ya kuelekea kwenye utulivu, kama ambavyo Epictetus anatuambia ni kuachana na mambo yote ambayo yapo nje ya uwezo wako, kutokuchukulia chochote milki yako na kujisalimisha kwa Mungu na mfumo wa asili.

Tunapaswa kujikumbusha hili pale tunapoamka, mchana na hata kabla ya kulala. Kwa sababu ni rahisi sana kujisahau, ukaanza kutaka kila kitu kiende kama unavyotaka wewe na hivyo kuumia pale vitu vinapoenda tofauti. Pia mara nyingi huwa tunajisahau na kujimilikisha kila kitu kama mali yetu, ni mpama tunapovipoteza ndiyo tunaumia sana.

Lakini unapojua kwamna huwezi kudhibiti kila kitu na hivyo kila kitu hakiwezi kwenda kama unavyotaka. Na unapojua kwamba huna unachomiliki, maana muda wowote unaweza kukipoteza, unakuwa na maisha yenye utulivu na furaha kubwa.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujikumbusha hudhibiti kila kitu na humiliki chochote.

#UpachaWaUdhibiti #JisalimisheKwaNguvuKuu #HakunaUnachomiliki

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,

Kocha Dr Makirita Amani,

http://www.amkamtanzania.com/kocha