“I am your teacher and you are learning in my school. My aim is to bring you to completion, unhindered, free from compulsive behavior, unrestrained, without shame, free, flourishing, and happy, looking to God in things great and small—your aim is to learn and diligently practice all these things. Why then don’t you complete the work, if you have the right aim and I have both the right aim and right preparation? What is missing? . . . The work is quite feasible, and is the only thing in our power. . . . Let go of the past. We must only begin. Believe me and you will see.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 2.19.29–34

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine mpya ambayo tumepata nafasi ya kuiona.
Ni siku bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo bora sana.

Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari UNACHOHITAJI NI KUANZA….
Rafiki, unajifunza mambo mengi sana na mazuri kwenye maisha yako,
Hapa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unajifunza mambo makubwa na mazuri sana, ambayo kama ukiyafanyia kazi maisha yako lazima yawe bora sana.
Lakini kama ilivyo kawaida ya binadamu, wengi hujifunza lakini hawachukui hatua.
Hivyo swali ni kwa nini huchukui hatua?
Kwa nini huyaweki kwenye matendo yale unayojifunza?

Unajifunza misingi muhimu ya kuendesha maisha yako,
Unajifunza tabia muhimu za kuishi kila siku,
Unajifunza namna bora ya kufanya kazi na biashara yako,
Unajifunza mbinu zote muhimu za kuboresha mahusiano na wengine,
Unajifunza namna ya kubomoa tabia zisizo nzuri kwako,
Lakini kwa nini huchukui hatua? Kwa nini huyaweki kwenye matendo yake unayojifunza?

Hili ni swali muhimu sana la kujiuliza na kutafakari kila siku kama ambavyo Epictetus anatuuliza kwenye tafakari hii ya leo.
Na anatuambia kitu kimoja, unachohitaji ni kuanza, mengine yatajipanga yenyewe.
Wengi hukwama kuanza kwa sababu huona mbele patakuwa pagumu sana.
Lakini hupaswi kuangalia mbele na kupafanya pakukwamishe.
Unachopaswa kufanya ni kuanza kuchukua hatua sasa, na ukishachukua hatua, mengine yatafuata yenyewe.
Hata utakapokutaha na ugumu, njia zotajitokeza zenyewe.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki, siku ya kuweka kwenye matendo yale yote unayojifunza, siku ya kuanza kuchukua hatua na yanayofuata yatakwenda sawa.
#ChukuaHatua, #WekaKwenyeMatendo, #WeweAnzaTu

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha