“Your principles can’t be extinguished unless you snuff out the thoughts that feed them, for it’s continually in your power to reignite new ones. . . . It’s possible to start living again! See things anew as you once did—that is how to restart life!”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 7.2

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari; WASHA UPYA FIKRA ZAKO…
Kama hutaki kuisahau misingi uliyochagua kuiishi kila siku, basi unapaswa kuwa unawasha upya fikra zako kila siku.
Kila siku unapaswa kuchochea fikra zako kwa yale unayoyataka kwenye maisha yako.

Kama hutaki kuchoka kile unachofanya, kama hutaki kuzoea kile unachofaya unapaswa kutengeneza fikra mpya kila wakati.
Tunapoanza kufanya kitu kipya huwa tunakuwa na hamasa kubwa, kwa sababu tunakuwa na fikra mpya kwenye kila tunachoanza.
Lakini muda unavyozidi kwenda, tunazoea kitu kile na hatupati tena ile hamasa tuliyokuwa nayo mwanzo.
Hii inatokana na kukosa fikra mpya kwenye kitu hicho, tunaendelea na fikra zile zile tulizoanza nazo.

Kama unataka kuishi upya, kama unataka kila wakati kuwa na hamasa na usichoke chochote, basi washa upya fikra zako kila siku.
Kwenye kila unachofanya, njoo na fikra mpya, fikra za kibunifu kila siku.
Na hizi zitawasha upya moto wa hamasa ndani yako, moto utakaokusukuma ufanye zaidi na zaidi kila siku.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwasha upya hamasa yako kwa kutengeneza fikra mpya kwenye kila unachofanya.
#WashaFikra, #AchaMazoea, #ChocheaFikraMpya

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha