“What’s left to be prized? This, I think—to limit our action or inaction to only what’s in keeping with the needs of our own preparation . . . it’s what the exertions of education and teaching are all about—here is the thing to be prized! If you hold this firmly, you’ll stop trying to get yourself all the other things. . . . If you don’t, you won’t be free, self-sufficient, or liberated from passion, but necessarily full of envy, jealousy, and suspicion for any who have the power to take them, and you’ll plot against those who do have what you prize. . . . But by having some self-respect for your own mind and prizing it, you will please yourself and be in better harmony with your fellow human beings, and more in tune with the gods—praising everything they have set in order and allotted you.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 6.16.2b–4a
Tuna siku nyingine mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Ni fursa ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari; KITU PEKEE UNACHOPASWA KUKITUKUZA…
Tumekuwa tunasumbuka na maisha kwa sababu tunahangaika na vitu vingi ambavyo havina maana yoyote kwetu.
Tunakimbizana na kila kitu kipya, siyo kwa sababu tunakihitaji hasa, ila kwa sababu hatutaki kupitwa au kwa kuwa kila mtu anakimbizana na kitu hicho.
Hii ndiyo hali inayozaa wivu, chuki, na kutokujiamini kwenye maisha yako.
Tuzo pekee unayohitaji kwenye maisha yako ni kuweza kuitumia vizuri akili yako na kudhibiti fikra zako. Ukiweza kufanya hili, utaweza kupata chochote unachotaka na pia unafurahia kila kinachoendelea kwenye maisha yako.
Kwa kuwa na umiliki wa akili yako na kudhibiti fikra zako, utaweza kuzipeleka kwenye yale muhimu zaidi na hivyo kukuondoa kwenye kupoteza muda kwa mambo yasiyokuwa na umuhimu wowote kwako.
Kitu pekee unachopaswa kukitukuza ni akili na fikra zako, mengine yote ni matokeo ya akili na fikra zako. Ukitukuza matunda na kusahau kinachozaa matunda, unajiweka kwenye nafasi ya kujiangusha mwenyewe. Kwa sababu matunda yatakapokoma, utakuwa hujui chanzo chake na hivyo kuwa kwenye hali isiyo nzuri.
Tukuza akili na fikra zako, na mengine yote yatakwenda kama unavyotaka wewe.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutukuza akili na fikra zako ili ziweze kukupa kile unachotaka.
#TukuzaFikra, #KazanaNaChanzoSiyoMatokeo, #FikraNdiyoChanzoKikuu
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani, http://www.amkamtanzania.com/kocha