“There are three areas in which the person who would be wise and good must be trained. The first has to do with desires and aversions—that a person may never miss the mark in desires nor fall into what repels them. The second has to do with impulses to act and not to act—and more broadly, with duty—that a person may act deliberately for good reasons and not carelessly. The third has to do with freedom from deception and composure and the whole area of judgment, the assent our mind gives to its perceptions. Of these areas, the chief and most urgent is the first which has to do with the passions, for strong emotions arise only when we fail in our desires and aversions.
—EPICTETUS, DISCOURSES, 3.2.1–3a

Ni siku nyingine mpya na ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana kwetu.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari MAENEO MATATU YA KUPATA MAFUNZO. . .
Epictetus anatuambia yapo maeneo matatu muhimu ambayo tunapaswa kupata mafunzo ili maisha yetu yaweze kuwa bora na tuwe na hekima.

Eneo la kwanza ni la hisia, hisia za matamanio na za chuki. Kuna vitu tunatamani kuvipata na kuna ambavyo tunakazana kuvikwepa. Tunapaswa kupata kile tunachotaka na kuepuka kuanguka kwenye kile tunachokwepa.

Eneo la pili ni msukumo wa kuchukua hatua, kwa tunachofanya au kutokufanya. Tunapaswa kujisukuma kuchukua hatua ambazo ni sahihi kwa kile tunachotaka, na siyo tu kufanya kwa mazoea au kwa kuwa inabidi ufanye.

Eneo la tatu ni fikra na maamuzi, tunapaswa kutengeneza mtazamonna taswira sahihi kwenye akili zetu ili tuweze kufanya maamuzi sahihi kwenye maisha yetu.

Haya ni maeneo matatu muhimu sana ambayo kama ukijifunza na kuyasimamia vizuri, utaweza kujijengea nidhamu ya kuendea kile unachotaka na kukipata.

Maeneo haya matatu yapo ndani ya uwezo wako na haijalishi uko wapi, unaweza kujifunza na kuyadhibiti vizuri.
Kaiendee siku ya leo kwa kujifunza na kuyadhibiti maeneo hayo.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kudhibiti hisia zako, kujisukuma kufanya yaliyo sahihi na kufikiri kwa kina na kufanya maamuzi sahihi.
#PataUnachotaka, JisukumeKufanya, FikiriKwaKina

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha