“If you wish to improve, be content to appear clueless or stupid in extraneous matters—don’t wish to seem knowledgeable. And if some regard you as important, distrust yourself.”
—EPICTETUS, ENCHIRIDION, 13a

Siku mpya,
Siku bora na siku ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi nyingine nzuri na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari; HUHITAJI KUJUA KILA KINACHOENDELEA…
Kwa dunia tunayoishi sasa, dunia ambayo tumeunganishwa kwa masaa 24 kwa kila kinachoendelea, dunia ambayo tukio lolote linalotokea kila mtu anaweza kulijua muda huo huo, ni dunia yenye mtego mkali sana.

Ni dunia ambayo bi rahisi kufikiri kwamba lazima ujue kila kinachoendelea, hupaswi kupitwa na habari yoyote mpya au kinachoendelea kwenye maisha ya wengine.
Na mitandao ya kijamii ndiyo inachochea zaidi moto huu wa kutaka kujua kila kinachoendelea.

Lakini kama unataka kupiga hatua, kama unataka utulivu wa nafsi na muda wa kufikiri kwa kina yale muhimu kwako, basi huhitaji kujua kila kinachoendelea.
Lazima uwe tayari kuonekana mjinga au kusema hujui kwa baadhi ya mambo.
Hakuna ubaya wowote kwako kwa kutokujua kila kinachoendelea kwenye maisha ya wengine au kwenye habari.
Hakuna ubaya wowote kwenye kusema sijui au sijali yale ambayo hayana umuhimu kwako, hata kama kila mtu anahangaika nayo.

Kwa wingi wa yale ambayo watu wanasumbuka nayo sasa, utajipe uhuru mkubwa sana kama utakuwa tayari kuachana nayo na kukubali kuonekana mjinga au usiyejua.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuachana na yale yote ambayo hayana umuhimu kwako na kuwa tayari kuonekana mjinga au usiyejua.
#SiyoLazimaKujuaKilaKitu, #HangaikaNaYanayokuhusu, UsiogopeKusemaSijui

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha