“Cato practiced the kind of public speech capable of moving the masses, believing proper political philosophy takes care like any great city to maintain the warlike element. But he was never seen practicing in front of others, and no one ever heard him rehearse a speech. When he was told that people blamed him for his silence, he replied, ‘Better they not blame my life. I begin to speak only when I’m certain what I’ll say isn’t better left unsaid.’”
—PLUTARCH, CATO THE YOUNGER, 4
Siku mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu,
Tunapaswa kushukuru kwa nafasi hii nyingine nzuri na ya kipee kwetu tuliyoipata leo.
Tukiweza kuitumia siku hii vyema na kufanya yale ambayo ni muhimu, tutaweza kupiga hatua sana kwenye maisha yetu.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari WAKATI SAHIHI WA KUONGEA…
Tunaishi kwenye zama ambazo watu wanaongea sana, na tukisema kuongea tunakuwa hatusemi sahihi, badala yake watu wanaropoka sana.
Watu hawawezi kutulia na chochote zama hizi, iwe ni kwenye maisha yao binafsi au mambo ya wengine, watu wanaropoka sana.
Kuongea na kuropoka huku kumekuwa kikwazo kwa wengi kupata wanachotaka na pia kumesababisha mahusiano ya wengi kuvunjika.
Kuongea sana pia kumewafanya wengi kupoteza heshima zao kwa wengine.
Kwa sababu kadiri unavyoongea sana, ndivyo inavyokuwa rahisi kuanika upumbavu uliopo ndani ya mtu.
Kama Cato anavyotuambia, wakati sahihi wa kuongea ni pale ambapo kuongea ni bora kuliko kukaa kimya. Pale ambapo ulichonacho ni muhimu sana na hakipaswi kuachwa bila ya kusemwa.
Huo ndiyo wakati sahihi wa kuongea, na kama ukifuata utaratibu huo, utagundua ni mara chache sana unahitaji kuongea, kwa sababu mara nyingi unayosukumwa kuyaongea siyo muhimu sana, kwamba yasiposemwa basi patakuwa na pengo kubwa.
Kadiri unavyopunguza kuongea yasiyo muhimu, ndivyo unavyojipa muda na nguvu za kufanya yale muhimu zaidi kwako.
Ongea pale tu inapokuwa muhimu zaidi kuongea na ulichonacho hakipaswi kuachwa kimya.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuongea pale unapopaswa kuongea na kuepuka kuropoka kama wengi wanavyofanya.
#UngeaInapokuwaMuhimu, #KukaaKimyaNiBusara, #SiyoLazimaUweNaMaoniKwaKilaKitu
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha