“The person is free who lives as they wish, neither compelled, nor hindered, nor limited—whose choices aren’t hampered, whose desires succeed, and who don’t fall into what repels them. Who wishes to live in deception—tripped up, mistaken, undisciplined, complaining, in a rut? No one. These are base people who don’t live as they wish; and so, no base person is free.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 4.1.1–3a
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana tuliyoiona leo.
Ni fursa ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KUJITAMBUA NI UHURU…
Yupo huru mtu yule ambaye anaishi kama anavyotaka, bila ya kulazimishwa, kuzuiwa au kujiwekea ukomo.
Yule ambaye anafanya yaliyo muhimu kwake na halazimiki kufanya yasiyo muhimu.
Yupo huru yule ambaye anaweza kukataa kutokufanya kile ambacho siyo muhimu, hata kama wengine wanafanya.
Yupo huru yule ambaye halalamiki kwa chochote kinachotokea au anachokutana nacho, badala yake anachukua hatua sahihi.
Watu wengi wanapoteza uhuru wa maisha yao kwa kujipa majukumu ambayo hayana umuhimu wowote kwao, ila wanakubali tu ili kuwaridhisha wengine.
Ukitaka kuishi maisha kumridhisha kila mtu, unaishia kutokumridhisha yeyote na mbaya zaidi maisha yako yanakuwa hovyo.
Kujitambua ni uhuru mkubwa sana kwenye maisha, kujua yale muhimu kwako na kuzingatia hayo, huku ukiachana na yale yasiyo muhimu.
Ukijitambua, huwi na haja ya kutaka kuwaridhisha wengine, bali wale waliojitambua watafurahi kuwa karibu na wewe.
Jitambue wewe mwenyewe kwanza, jijue kwa undani, yapi muhimu na yenye maana kwako kufanya na weka juhudi zako kwenye hayo.
Kama kitu siyo muhimu, kama kitu husukumwi kukifanya usifanye. Hakuna mtu muhimu kumridhisha zaidi yako wewe.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujitambua na kufanya yale ambayo ni muhimu pekee.
#KujitambuaNiUhuru, #FanyaYaliyoMuhimu, #UsimfurahisheKilaMtu
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha