Ni kitu ambacho kiliondoka na vita kuu ya pili ya dunia.

Katika zama tunazoishi sasa, hakuna unachoweza kujifunza mara moja na ukawa umeshajua kiasi cha kutosha na ukawa huhitaji kujifunza tena.

Chochote unachojifunza leo, siku siyo nyingi zijazo kuna maarifa mapya yatakayotoka, ambayo yanafanya ulichojifunza leo kisiwe sahihi tena.

Katika zama zilizopita ilikuwa ukijifunza kitu unaweza kukitumia kwa muda mrefu, kwa sababu mabadiliko yalitokea kwa kasi ndogo sana. Lakini sasa hivi mabadiliko yanatokea kwa kasi kubwa, maarifa mapya na bora yanagunduliwa na kuzalishwa kila siku.

Hivyo pamoja na kazi au biashara yako ambayo inakutaka muda wako mwingi, una jukumu jingine kubwa la kuendelea kujifunza kila siku. Pia unapaswa kuwa na uvumilivu wa kukubali kwamba unachojua sasa siyo sahihi au kimepitwa na wakati, hata kama kwa sasa kinakulipa. Maana kukataa hilo kutakuwa kikwazo kwako baadaye.

Kujifunza ni jukumu lako la kila siku, na ni sehemu muhimu sana ya mafanikio yako, ipe muda wa kutosha.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha