“. . . freedom isn’t secured by filling up on your heart’s desire but by removing your desire.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 4.1.175
Ni siku nyingine mpya na ya kipekee sana kwetu.
Tumepata nafasi bora kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari UHURU NI BURE…
Hauwi huru kwa kupata kila unachotaka, bali unakuwa huru pale unapotaka vitu vichache zaidi.
Unakuwa huru pale unapodhibiti tamaa zako na kutokuweka furaha yako kwenye vitu unavyotaka.
Hii ndiyo maana tunasema uhuru ni bure, kwa kuwa ukiondoa tamaa zako, ukiacha kujiambia lazima upate vitu fulani ndiyo uwe na furaha, ndivyo unavyozidi kuwa huru.
Utumwa una kazi, unaanza kwa kujiwekea mahitaji mengi, kisha kujiambia utakuwa na furaha ukishayapata.
Tatizo ni unapoyapata unagundua kuna mengine zaidi ya kupata, hivyo unaahirisha tena furaha yako. Utaenda hivyo maisha yako yote, usipate kila unachotaka na hivyo kutokuwa huru na kukosa furaha.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwa huru kwa kuwa na mahitaji machache.
#UhuruNiBure, #UtumwaNiKazi #DhibitiTamaaZako
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha