“Drama, combat, terror, numbness, and subservience—every day these things wipe out your sacred principles, whenever your mind entertains them uncritically or lets them slip in.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 10.9
Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KUWA MAKINI NA UNACHORUHUSU KIINGIE KWENYE AKILI YAKO…
Kila kitu tunachoruhusu kiingie kwenye akili zetu, huwa kinaacha doa fulani katika akili.
Hivyo tunaporuhusu vitu ambavyo siyo vizuri, vinaacha madoa ambayo siyo mazuri.
Ukiruhusu mazoea, hofu na mawazo mengine hasi kuingia kwenye akili yako, hayo ndiyo mambo yatakayotokea kwenye maisha yako.
Lakini kama utaruhusu mawazo chanya pekee yaingie, utapata matokeo chanya kwenye maisha yako.
Ni mara ngapi umewahi kupata wazo fulani kubwa sana na lenye matokeo makubwa kwa baadaye. Ukalifikiria wazo hilo na kuona linawezekana kabisa.
Ukaenda kwa mru wako wa karibu ukiwa na hamasa ya hali ya juu na kumweleza wazo hilo. Halafu anaanza kulichambua hatua kwa hatua kwa nini haliwezekani,
Je unatoka hapi ukiwa na hali gani? Unatoka ukiwa na hamasa ya kufanikiwa zaidi au unatoka umekata tamaa?
Wengi hutoka kwenye hali kama hiyo wakiwa wamekata tamaa kabisa na kuachana na kile walichokuwa wanafikiria.
Tatizo linakuwa limeanzia pale mtu unaporuhusu fikra hasi kuingia kwenye akili yako.
Tunaishi kwenye mazingira ambayo tumezungukwa na watu hasi pamoja na fikra hasi. Hivyo ni rahisi sana kuambukizwa fikra hizi kaja ilivyo rahisi kuambukizwa mafua.
Unapaswa kuwa na kinga muhimu sana ya kiakili ili kuchuja kila kinachoingia kabla hakijaleta madhara.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuchuja kila kinachotaka kuingia kwenye akili yako ili kisilete madhara hasi.
#DhibitiFikraZako, #ChujaKilaKinachoingia, #SimamiaMaishaYako
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha