“Pay close attention in conversation to what is being said, and to what follows from any action. In the action, immediately look for the target, in words, listen closely to what’s being signaled.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 7.4

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari ANGALIA KISABABISHI NA MATOKEO…
Chochote kinachotokea kwenye maisha yetu, huwa tunakazana kuyaangalia matokeo na kusahau kabisa kuangalia kisababishi.
Tunachosahau ni kwamba hakuna kitu kinachotokea kama ajali au kwa bahati tu.
Kila kinachotokea kina kisababishi chake.
Na hivyo kama tunataka kuelewa matokeo tunayopata, na kama tunataka kuyabadili kwa namna yoyote ile, basi tunapaswa kujua kisababishi.
Ni kwenye kisababishi ndipo tunapoweza kubadili chochote kinachoendelea kwenye maisha yetu.

Usihangaike sana na matokeo, hangaika zaidi na kile kinachozalisha matokeo hayo. Hapo ndipo nguvu ya mabadiliko na haya nguvu ya kuboresha zaidi ilipo.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuangalia kisababishi na siyo matokeo pekee.
#KilaKituKinaKisababishi, #UsihangaikeNaMatokeoPekee, #UsitafuteMajibuRahisiKwaMamboMagumu

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha