“Here’s a way to think about what the masses regard as being ‘good’ things. If you would first start by setting your mind upon things that are unquestionably good—wisdom, self-control, justice, courage—with this preconception you’ll no longer be able to listen to the popular refrain that there are too many good things to experience in a lifetime.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 5.12

Ni siku nyingine mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu,
Ni nafasi nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari UZURI WA KWELI NI RAHISI…
Tumekuwa tunatafuta uzuri kwa gharama kubwa sana,
Tumekuwa tunakazana sana ili kuwa na maisha mazuri, kazi nzuri, biashara nzuri na hata mahusiano bora.
Lakini gharama zozote tunazoingia katika kutafuta uzuri kwenye maeneo hayo ya maisha, ni gharama ambazo tumechagua wenyewe kuzipoteza.

Uzuri halisi, uzuri wa kweli ni rahisi na hauna gharama.
Wastoa wanatuambia, kama tunataka kuwa na maisha mazuri, kama tunataka kila eneo la maisha yetu liende vizuri, basi tunahitaji vitu vinne tu;
Moja; hekima, ambayo unaipata kwa kujifunza na kufanyia kazi unayojifunza na kuweza kuchukua hatua sahihi mara zote.
Mbili; kujidhibiti mwenyewe, kujua yaliyo ndani ya uwezo wako na yaliyo nje ya uwezo wako.
Tatu; kuwa mtu wa haki, kwa kufanya kile kilicho sahihi mara zote.
Nne; kuwa na ujasiri wa kujaribu vitu vipya, kwenda hatua ya ziada na kufanya kwa utofauti.

Vitu hivyo vinne, ni rahisi kwa kila mmoja wetu, huhitaji kuwa na chochote cha ziada ili kuweza kuvifanyia kazi vitu hivyo vinne.
Hivyo unaweza kuona ni jinsi gani uzuri wa kweli ni rahisi, kazi ni kwetu kuchukua hatua.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuishi kwa misingi rahisi ya uzuri ambayo ni hekima, kujidhibiti, haki na ujasiri.
#UzuriNiRahisi, #DhibitiHisiaZako #HekimaUdhibitiHakiUjasiri

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha