“When your sparring partner scratches or head-butts you, you don’t then make a show of it, or protest, or view him with suspicion or as plotting against you. And yet you keep an eye on him, not as an enemy or with suspicion, but with a healthy avoidance. You should act this way with all things in life. We should give a pass to many things with our fellow trainees. For, as I’ve said, it’s possible to avoid without suspicion or hate.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 6.20
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari MAISHA KAMA MCHEZO…
Katika mazoezi au mchezo wowote, wachezaji huwa wanachukulia kila kinachotokea kama sehemu ya mchezo.
Mchezaji mmoja anapomwamgusha mchezaji mwingine, hachukulii kama ugomvi na kuweka vinyongo na kupanga kulipa kisasi, anachukulia kama sehemu ya mchezo na mambo yanaendelea.
Lakini inapotokea kwenye maisha ya kawaida, mtu amepishana kidogo na wewe, au kukukwamisha kwenye jambo lolote, unapata hasira na kutaka kulipa kwa kile anachofanya.
Vipi kama utachukulia maisha kama mchezo, kwa kuona kile wanachofanya wengine kama sehemu ya mchezo na kutokukasirika wala kupanga kulipa kisasi?
Vipi kama unaianza siku yako ukitegemea kuna watu watakwenda kinyume na unavyotaka, watakuudhi na hata wengine kukuangusha, lakini ukachukulia hilo kama sehemu ya mchezo?
Kwa hakika maisha yatakwenda vizuri na hakuna yeyote atakayekusumbua.
Chukulia maisha yako kama mchezo, na kila kinachotokea kama sehemu ya mchezo na utakuwa na amani na utulivu wakati wowote.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuyachukulia maisha kama mchezo na kuwa na amani na utulivu mkubwa.
#MaishaNiMchezo, #UsiumizweNaChochote, #TegemeaWatuKwendaTofauti
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha