“Just as what is considered rational or irrational differs for each person, in the same way what is good or evil and useful or useless differs for each person. This is why we need education, so that we might learn how to adjust our preconceived notions of the rational and irrational in harmony with nature. In sorting this out, we don’t simply rely on our estimate of the value of external things, but also apply the rule of what is in keeping with one’s character.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 1.2.5–7
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari JENGA TABIA YAKO…
Tabia yako ndiyo silaha yako katika mapambano ya kuwa na maisha bora.
Ili uweze kushinda mapambano haya, lazima ujijengee tabia bora na imara.
Na ili ujijengee twbia bora na imara, lazima uchukue muda na kujifunza.
Watu wengi wanaendesha maisha kwa mazoea, kwa kufanya yale ambayo wamezoea kufanya, yale ambayo wengine wanafanya.
Kwa kuendesha maisha kwa mazoea, lazima utafanya makosa mengi sana, utawapa wengine nafasi ya kukutumia wewe watakavyo.
Mazoea mengi huwa ni maoni na siyo uhalisia.
Mtazamo wa kilicho sahihi na kisicho sahihi, kizuri na kibaya, muhimu na isiyo muhimu, ni tofauti kwa kila mtu. Na ndiyo maana kuna mkanganyiko mkubwa sana.
Wengine wanakuambia hiki ndiyo sahihi, wengine wanakuambia siyo sahihi.
Wapo watakaokuambia kufanya hivi ni vizuri, wengine watakuambia ni vibaya.
Hivyo kujua ambacho ni sahihi au siyo sahihi kwako, muhimu au siyo muhimu, lazima uchukue muda kujifunza kuhusu wewe mwenyewe.
Lazima kwanza ujenge tabia yako bora, ambayo itakuongoza kwenye yapi sahihi na siyo sahihi na yapi muhimu na siyo muhimu.
Hutakuwa na maisha bora kwa kufanya vitu kwa mazoea,
Hutakuwa na maisha bora kwa kufanya kile ambacho kila mtu anafanya.
Utakuwa na maisha bora kwa kujijua wewe mwenyewe na kisha kujenga tabia imara zitakazokuongoza kwenye maisha yako.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujijengea tabia bora za kukuongoza kwenye maisha yako.
#TabiaNdiyoMsingi, #UsiishiKwaMazoea, #KujifunzaHakunaMwisho
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha