“Let us therefore set out whole-heartedly, leaving aside our many distractions and exert ourselves in this single purpose, before we realize too late the swift and unstoppable flight of time and are left behind. As each day arises, welcome it as the very best day of all, and make it your own possession. We must seize what flees.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 108.27b–28a
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari MILIKI SIKU YAKO…
Maisha yetu yote yako ndani ya siku moja.
Jinsi tunavyoiishi siku moja, ndivyo tunavyoishi siku nyingine zote na ndivyo tunavyoyaishi maisha yetu.
Ni rahisi kuipoteza siku moja na usione madhara yake, lakini usichojua ni kwamba, kwa kupoteza siku moja, na nyingine na nyingine tena ndivyo unavyoyapoteza maisha yako.
Kama hutaki kupoteza maisha yako basi hatua ya kwanza ni kuimiliki siku yako.
Unaimiliki siku yako kwa kuipangilia tangu unapoianza mpaka unapoimaliza.
Andika kabisa ni vitu gani utafanya na kwa wakati gani.
Weka sawa vipaumbele vyako na hivyo ndiyo viwe vitu vya kwanza kufanya kwenye siku siku yako.
Iendeshe siku yako kwa ratiba na utaratibu wako na siyo kwa matukio.
Usivunje ratiba na utaratibu uliojiwekea kwa sababu ya matukioa mbalimbali yanayoendelea.
Kuwa mkali sana kwenye umiliki wa siku yako, usiruhusu usumbufu wa aina yoyote ile uingie kwenye siku yako.
Usiruhusu hata sekunde chache kupotea kwenye siku yako.
Kumbuka unayo siku hii kwa wakati huu pekee, ikishapita imepita, huwezi kuipata tena.
Hivyo imiliki na kuisimamia vizuri, kisiwepo chochote cha kuvuruga ratiba na mpangilio wako wa siku,
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuimiliki siku yako, kufuata ratiba na utaratibu wako, siku ya kuishi kwa vipaumbele vyako na siyo matukio.
#MilikiSikuYako, #UsiishiKwaMatukio, #MudaHaurudiNyuma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha