“Those obsessed with glory attach their well-being to the regard of others, those who love pleasure tie it to feelings, but the one with true understanding seeks it only in their own actions. . . . Think on the character of the people one wishes to please, the possessions one means to gain, and the tactics one employs to such ends. How quickly time erases such things, and how many will yet be wiped away.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 6:51, 59
Hongera sana mwanamafanikio kwa nafasi hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni fursa bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KAZANA KUWEKA JUHUDI…
Watu wengi wamejigeuza kuwa watumwa wao wenyewe, kwa kufanya vitu ili waonekane au kwa kitegemea kupata furaha baada ya matokeo ya kile wanachofanya.
Hivyo watu wanaweka mkazo mkubwa kwenye namna ambavyo wengine wanawachukulia au nini wanakwenda kupata.
Kuweka mkazo kwenye vitu hivi vya nje kumekuwa kunawaangusha wengi, kwa sababu mambo hayatokei kama tunavyopanga na siyo kila mtu anakubaliana na tunachofanya.
Hivyo basi, sehemu pekee ya wewe kuweka mkazo ni kwenye juhudi unazoweka, hatua unazochukua.
Kazana kuweka juhudi, fanya kwa sababu unataka kufanya, kwa sababu ni muhimu kwako kufanya na kwa sababu ndiyo kitu sahihi kufanya.
Kwa kuweka mkazo kwenye ufanyaji, na kuachana na mambo ya nje, mara zote utapata matokeo ambayo ni bora sana kwako.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kukazana kuweka juhudi na siyo kuhangaika na mambo ya nje.
#KazanaKuwekaJuhudi, #UsitakeKumfurahishaKilaMtu, #UsiwekeFurahaKwenyeMatokeo
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha