Mfalme mmoja alikuwa na binti yake ambaye alikuwa anata kumuoza. Aliwakusanya vijana wote wa ufalme wake na kuwaeleza kwamba anatafuta kijana ambaye anaweza kumuoa binti yake, ambaye pia atarithi ufalme huo hivyo lazima awe imara.

Akawapa sharti moja, kwamba kijana atakayeweza kuvuka kwenye bwawa ambalo lina mamba wakali na akatoka akiwa hai basi ataweza kuchagua kupewa fedha nyingi, kupewa sehemu kubwa ya ardhi au kumuoa binti mfalme na hivyo kuridhi sehemu ya ufalme. Aliwaeleza hilo wakiwa pembeni ya bwawa hilo ambalo mamba walikuwa wanaonekana wakipita, huku wakiwa na njaa.

Kabla mfalme hajamaliza kuongea, alisikia kishindo kikubwa kwenye maji na muda mchache baadaye kuna kijana aliibukia upande wa pili wa bwawa huku akiwa anahema kweli, aliweza kuogelea na kuvuka bwawa lile ndani ya muda mfupi mno.

sight like an alligator

Mfalme alimwita na kumpa pongezi kwa ujasiri wake mkubwa wa kuvuka bwawa lenye mamba hao wakali sana. Mfalme akamuuliza kijana, je unataka nikupe fedha nilizoahidi? Kijana akasema hapana mfalme. Akamuuliza tena je unataka nikupe sehemu kubwa ya ardhi, akajibu hapana mfalme. Basi mfalme akasema kwa kuwa hutaki fedha wala ardhi, basi nafikiri utakuwa umechagua kumuoa binti yangu kipenzi na hivyo utarithi ufalme huu, kijana akajibu hapana mfalme.

Mfalme alishangazwa, na kwa hali ya kuduwaa akamuuliza kijana, sasa wewe unataka nini? Kijana akamjibu, nataka kujua ni nani aliyenisukumia kwenye hilo bwawa lenye mamba wakali.

Naamini uko vyema rafiki yangu, ukiendelea kuchukua hatua na kuweka juhudi kubwa ili uweze kupata matokeo bora sana.

Kwa hadithi hii nzuri tuliyoanza nayo leo, kuna somo kubwa sana la kujifunza hapo, licha ya kijana kuweza kuvuka bwawa lenye mamba wakali, hakuweza kufanya hivyo peke yale, badala yake alisukumwa na mtu kuweza kufanya hivyo.

Kwa maamuzi yake peke yake angeingiwa na hofu na kujiona hawezi na hivyo asingejaribu, lakini kwa kusukumwa na mtu mwingine na kujikuta tayari yupo kwenye maji, hakuwa na namna bali kuchukua hatua ili kunusuru maisha yake.

Tunaweza kusema kwamba hamasa ndiyo ilimwezesha kijana huyo kuvuka bwawa lenye mamba wakali na kutoka salama.

Rafiki, hamasa ni kitu ambacho watu wengi hawajakielewa, lakini ni kitu muhimu sana kwa mafanikio yetu. Bila ya hamasa huwezi kupiga hatua yoyote kubwa.

Watu wengi wamekuwa wanasumbuka sana na hamasa, mwanzo wanapoanza kitu wanakuwa na hamasa ya hali ya juu, hamasa hiyo inawasukuma kujituma sana na hapo wanapata matokeo mazuri. Baada ya kuanza kupata matokeo hayo mazuri, wengi wanaanza kuyazoea na hamasa waliyokuwa nayo inaanza kushuka. Hamasa ikishashuka hawapati tena matokeo makubwa na hapo maisha yanakuwa ya mazoea na hakuna makubwa wanayofanya.

Rafiki, kama unataka hamasa ambayo inadumu kwa muda mrefu au kama unataka kurudisha hamasa ambayo imepotea, basi unahitaji kupata nafasi kama aliyoipata kijana wa kwenye hadithi niliyokushirikisha hapo juu. Unahitaji mtu wa kukusukuma uingie kwenye bwawa la maji yenye mamba wa kali.

Ila tu tofauti ni kwamba bwawa unaliogopa kuingia wewe halina mamba wanaoweza kuondoa maisha yako;

Huenda bwawa unaloogopa kuingia wewe ni biashara mpya ambayo unataka kuanza lakini kila wakati unaahirisha na kuona hujawa tayari. Unahitaji mtu wa kukusukuma kuingia kwenye biashara hiyo na ukishaingia utaweka juhudi kubwa ili usipate hasara.

Huenda bwawa lako ni kutaka kuikuza zaidi biashara yako, ambayo kwa kipindi kirefu imedumaa eneo moja. Lakini kila ukifikiria kuchukua hatua mpya unaona kama utapoteza kile ulichonacho sasa. Hapa unahitaji mtu wa kukusukuma kwenye kuchukua hatua hizo mpya ili uweze kukuza biashara hiyo.

Huenda bwawa lako ni kitabu unachotaka kuandika, kila wakati unajiambia utaandika kitabu lakini hupati muda wa kukaa chini na kutekeleza hilo. Unahitaji mtu wa kukusukuma uingie kwenye uandishi na upambane mpaka umalize kitabu.

Inawezekana pia kwamba bwawa lako ni malengo ambayo umekuwa unajiwekea kwa miaka mingi sasa. Kila mwanzo wa mwaka unaweka malengo hayo, lakini mwaka unaisha hujachukua hatua. Mwanzo mwingine wa mwaka unaweka tena malengo hayo, unachukua hatua kidogo hamasa inaisha na unarudi kwenye mazoea. Hapa unahitaji mtu wa kukusukuma kwenye malengo hayo na uweze kuyatimiza ili maisha yako yawe bora.

Yapo mabawa yanayowazuia wengi, mahusiano yenye migogoro, afya isiyo imara, tabia zinazokuzuia kufanikiwa, kazi unayofanya ambayo umekua hukui tena, muda usiokutosha kwa mengi unayotaka kufanya na kadhalika. Kwa kila hatua ambayo unataka kupiga lakini hupati msukumo wa kuchukua hatua, basi jua hilo ni bwawa lako, na unachohitaji ni mtu wa kukusukuma kuingia kwenye bwawa hilo ili uweze kubadili maisha yako.

Rafiki, najua swali unalojiuliza ni unapata wapi mtu huyo wa kukusukuma. Najua una mabwawa mengi ambayo yanakukwamisha kwenye maisha yako, na unajiambia laiti ningepata mtu wa kunisukuma hapa ningefika mbali sana.

Na hapo ndipo mimi Kocha wako ninapoingia kwenye mafanikio yako, hapo ndipo mimi na watu wengine tunakusukuma uingie kwenye hilo bwawa unalohofia, lakini pia tunakusaidia kuhakikisha unatoka ukiwa hai.

Rafiki yangu mpendwa, nimekuandalia programu ya GAME CHANGERS ambayo hii kazi yake ni moja, kukusukuma kufanya kile kitu ambacho umekwama kufanya kwa muda mrefu, kukusukuma ufanye kile ambacho umeshajiaminisha kwamba huwezi kufanya.

Hii ni programu yenye manufaa mawili kwa wakati mmoja, unapata msukumo kutoka kwa Kocha, lakini pia unapata msukumo kutoka kwa wenzako ambao nao wanataka kupiga hatua kama unavyotaka kupiga wewe. Hivyo kwa nguvu hizi kubwa mbili, utaweza kuingia kwenye bwawa lolote linalokusumbua na ukatoka ukiwa hai kabisa, tena ukiwa na nguvu kubwa zaidi kuliko ulivyoingia awali.

Programu hii ya GAME CHANGERS huwa inakuja mara chache sana, na safari hii inakujia mwezi Juni 2019, siku zote 30 za mwezi juni zitakuwa siku za kupata msukumo mkubwa kutoka kwenye programu hii. Na baada ya siku hizo 30, utakuwa na msingi sahihi wa kuendelea kujisukuma mwenyewe kwa kile ambacho unafanya na hata vitu vingine unavyopanga kufanya.

Zipo nafasi tano pekee za kushiriki kwenye programu hii, na sababu ya nafasi hizi kuwa chache sana ni ili Kocha aweze kupata muda wa kumfuatilia kila mmoja kwa undani. Pia kutakuwa na simu za pamoja kila wiki hivyo watu watano ndiyo wanaweza kuendea kwenye mazungumzo ya pamoja ya simu.

Gharama ya kushiriki programu hii ni tsh 300,000/= (shilingi laki tatu) kwa siku zote 30 utakazokuwa kwenye programu hii. Gharama hii ni kubwa kwa sababu thamani unayokwenda kuipata kwenye programu hii ni kubwa sana, utaweza kuondoka pale ulipokwama sasa na kupiga hatua sana. Kwa kiwango cha chini sana, faida utakayoipata kwenye maisha yako kwa kushiriki programu hii ni mara kumi ya kiwango ulicholipia, lakini pia inaweza kuwa mara mia au hata mara elfu. Tunasema uwekezaji pekee unaolipa sana ni ule wa kuwekeza ndani yako kwa kujifunza. Laini unapowekeza ndani yako ili kupata mwongozo sahihi, inalipa mara dufu.

Programu hii inaanza tarehe 01/06/2019 mpaka tarehe 30/06/2019. Mwisho wa kulipia ili uweze kushiriki programu hii ni tarehe 29/05/2019, baada ya hapo tarehe 30 Kocha atakuwa na mazungumzo na kila mtu aliyepata nafasi ya kushiriki programu hii. Tarehe 01/06/2019 programu itaanza na siku hiyo saa 12 jioni kutakuwa na mazungumzo ya kwanza ya simu ambapo kila mtu ataweka ahadi zake na mipango atakayofanyia kazi kwenye programu hii. Kila jumamosi saa 12 jioni kutakuwa na mazungumzo ya pamoja kwa simu na kila mtu ataeleza hatua alizopiga na hata changamoto alizokutana nazo.

Unapokuwa kwenye programu hii, kila siku kwa siku 30 utajifunza kanuni na miongozo ya kuweza kuwa GAME CHANGER wa kudumu kwenye maisha yako. kanuni na miongozo hii inatoka kwa wale ambao wameweza kupiga hatua kubwa sana kwenye maisha yao. Tunasema ukifanya kile ambacho waliofanikiwa wanafanya, utapata matokeo wanayopata. Hivyo utajifunza misingi sahihi ya kufikiri, kuamini na kuchukua hatua ambayo itakuwezesha kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.

Karibu sana rafiki yangu mpendwa kwenye programu hii ya GAME CHANGERS, programu hii ndiyo kitu pekee kitakachokusukuma wewe kuelekea kwenye ndoto zako. Kujihakikishia nafasi ya kushiriki programu hii, tuma ujumbe sasa kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 ukisema unataka kushiriki kwenye GAME CHANGERS, na utawekwa kwenye kundi maalumu la programu hii.

Nikukumbushe rafiki, nafasi za kushiriki programu hii ni chache sana ukilinganisha na wenye uhitaji. Nafasi ni tano pekee, lakini wenye uhitaji ni wengi. Hivyo kanuni rahisi itakayotumika ni anayewahi ndiye anayepata nafasi, zikishajaa basi ndiyo zimeisha. Hivyo kama hutaki kukosa nafasi hii, tuma ujumbe sasa kwa wasap na lipa ada mapema kabla ya tarehe 29/05/2019.

Mpaka sasa nafasi tatu za programu hii zimeshachukuliwa na wale waliotoa taarifa mapema, hivyo zimebaki nafasi mbili pekee. Kama hutaki kukosa programu hii, huu ndiyo wakati wako wa kuipata. Tuma ujumbe sasa kwa wasap kwenda namba 0717396253 ukisema utashiriki GAME CHANGERS na pia utoe tarehe unayotegemea kulipa ada ili usikose nafasi hii adimu.

Nakusubiri kwa hamu sana rafiki yangu kwenye programu hii, nikupe maarifa na misingi sahihi ya kuweza kuingia kwenye hilo bwawa unalohofia na uweze kuleta mabadiliko makubwa kwenye maisha yako. Usikose nafasi hii.

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,

Kocha Dr Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha