“What is your vocation? To be a good person.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 11.5
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri ya leo.
Ni siku mpya na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari JUKUMU LAKO KUU KWENYE MAISHA…
Jukumu lako kuu kwenye maisha ni KUWA MTU MWEMA.
Hilo ndiyo jukumu ambalo ulilikamilisha kwa usahihi, utakuwa na maisha bora na yenye mafanikio makubwa sana.
Unakuwa mtu mwema kwa kufanya kilicho sahihi mara zote,
Unakuwa mtu mwema kwa kujali maslahi ya wengine,
Unakuwa mtu mwema kwa kuishi kulingana na kanuni za asili.
Unakuwa mtu mwema kwa kuhakikisha kila unachogusa unakiacha kikiwa bora kuliko ulivyokikuta.
Hili ni jukumu ambalo kila mmoha wetu analiweza na kila mmoja wetu anapata fursa za kulitekeleza kila siku.
Kwenye kazi yako kuwa mwema kwa kufanya kazi bora na kuwahudumia wengine vizuri.
Kwenye biashara yako kuwa mtu mwema kwa kuwahudumia wateja wako kwa bidhaa/huduma sahihi na kuwajali.
Kwenye maisha yako kuwa mwema kwa kuwajali wengine na kuhakikisha maisha hyao yanakuwa bora zaidi kupitia wewe.
Ifanye kazi yako, na kazi yako kuu ni kuwa mtu mwema.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutekeleza jukumu lako kuu ya kuwa mtu mwema.
#MtuNiUtu, #FanyaKilichoSahihi, #BoreshaMaishaYaWengine
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1