“We cry to God Almighty, how can we escape this agony? Fool, don’t you have hands? Or could it be God forgot to give you a pair? Sit and pray your nose doesn’t run! Or, rather just wipe your nose and stop seeking a scapegoat.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 2.16.13
Siku mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari USILALAMIKE, CHUKUA HATUA SAHIHI…
Dunia haina usawa, hili limekuwa lalamiko la wengi.
Unaweza kukazana sana kupiga hatua, lakini wengine wananufaika kupitia kile unachofanya.
Unaweza kufanya kila unachopaswa kufanya, lakini matokeo yakaja tofauti na ulivyotegemea.
Watu watakuahidi vitu lakini hawatavitekeleza.
Wengine watakuumiza kwa yale wanayosema au kufanya.
Hivyo ndivyo dunia ilivyo, na haitabadilika kwa sababu yako wewe.
Ili kuwa na maisha tulivu, maisha bora ambayo hayayumbishwi na yanayotokea nje yako, unapaswa kuacha kuwa mtu wa kulalamika na kuchagua kuwa mtu wa kuchukua hatua sahihi.
Kama kuna kitu kimetokea ambacho hukipendi au hakubaliani nacho basi kibadili.
Na kama huwezi kukibadili basi achana nacho.
Kutumia kuda wako mwingi kulalamikia kitu kilichotokea hakutabadili kilichotokea, badala yake unakuwa umechangua kupoteza zaidi muda wako.
Kuwa mtu wa kuchukua hatua na hakuna kitakachoweza kukukwamisha kwa namna yoyote. Kwa sababu matokeo yoyote unayopata, yawe mazuri au mabaya, swali la kwanza kwako kujiuliza ni kipi sahihi kufanya katika wakati huo.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuchukua hatua na siyo kulalamika.
#UsiweMtuWaKulalamika, #KuwaMtuWaKuchukuaHatua, #MaraZoteFanyaKilichoSahihi
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1