“There is no vice which lacks a defense, none that at the outset isn’t modest and easily intervened—but after this the trouble spreads widely. If you allow it to get started you won’t be able to control when it stops. Every emotion is at first weak. Later it rouses itself and gathers strength as it moves along—it’s easier to slow it down than to supplant it.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 106.2b–3a
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari TATUA MATATIZO MAPEMA…
Tatizo lolote likiwa changa ni rahisi kulitatua,
Lakini kadiri tatizo hilo linavyokaa muda, linakua na kukomaa na inakuwa vigumu sana kulitatua.
Ni rahisi kupuuza tatizo likiwa dogo na kuona halina shida, lakini kadiri muda unavyokwenda, linakomaa na kuleta madhara makubwa.
Kuwa mtu wa kutatua matatizo na changamoto mapema kabla havijakomaa zaidi.
Chochote ambacho hakijakaa sawa kwenye maisha yako chukua hatua mapema kabla mambo hayajawa makubwa zaidi.
Usiache tatizo likue na kusambaa na baadaye kuwa kikwazo kikubwa zaidi kwako.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kitatua matatizo na changamoto mapema kabla hazijakomaa.
#TatuaTatizoMapema, #TatizoLinapokaaLinakuaKubwa, #WakatiWaKuchukuaHatuNiSasa
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1