“In this way you must understand how laughable it is to say, ‘Tell me what to do!’ What advice could I possibly give? No, a far better request is, ‘Train my mind to adapt to any circumstance.’ . . . In this way, if circumstances take you off script . . . you won’t be desperate for a new prompting.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 2.2.20b–1; 24b–25a
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari IJENGEE AKILI YAKO UWEZO…
Huwa tunapenda sana kuambiwa nini cha kufanya kwenye kila wakati,
Huwa tunapenda kuwa na maandalizi ya kutosha kwenye jambo lolote lile.
Na huwa tunapenda kuwa na majibu ya kila hali inayoweza kujitokeza.
Lakini hivyo sivyo maisha yanavyokwenda,
Mambo hayatokei kama tulivyotegemea,
Na maandalizi tunayokuwa nayo hayaendani na hali tunazokutana nazo.
Na hapa ndipo wengi wanapokwama na kuona mambo hayaendi.
Hapa wengi huona kama dunia inawatega na kuamua kuwatesa.
Lakini ukweli ni kwamba dunia inafanya yake, wala hata haina habari na wewe. Haijali kama hata upo au haupo.
Hivyo njia bora ya wewe kukabiliana na jinsi dunia inavyokwenda, kwa namna isiyotabirika, ni kuijengea akili yako uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi kwa hali unayokutana nayo.
Usikariri nini cha kufanya, kwa sababu hujui nini kitatokea, bali jijengee uwezo wa kufikiri kwenye chochote kinachotokea na utaweza kupata majibu sahihi.
Maisha ni kama hisabati, wanaofauli siyo wanaokariri majibu, bali wanaojua kanuni sahihi na kuweza kuzitumia kwa usahihi kwa kila swali gumu wanalokutana nalo.
Kanuni sahihi ya kufanikiwa kwenye maisha ni kuwa na uwezo mzuri wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujijengea uwezo mzuri wa kufikiri na kuacha kukariri.
#JijengeKifikra, #UsikaririMaisha #DuniaInafanyaYake
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1