Rafiki yangu mpendwa,

Nimekuwa nakuambia sana jambo hili moja kuhusu biashara, kwamba biashara ni kiumbe hai, ambacho kinazaliwa, kinakua au kudumaa na mwishowe kinakufa. Biashara ni kitu ambacho kina maisha yake ya kujitegemea na jinsi ambavyo kinapewa uhuru wake ndivyo inavyofanikiwa zaidi.

Lakini pia biashara huwa inakuwa na tabia zake, ambazo zinaweza kuifanya ifanikiwe zaidi au kuizuia isifanikiwe. Tabia hizi za biashara huwa zinatokana na tabia ambazo mwanzilishi wa biashara hiyo anazo

Na hii ndiyo maana kwenye kila biashara kuna utaratibu na utamaduni fulani uliopo, ambao huwa ni mgumu sana kubadilisha. Hata wafanyakazi wapya wanapokuja kufanya kazi kwenye biashara hiyo, baada ya muda hujikuta wameshavaa utamaduni huo wa biashara.

Utaratibu na utamaduni uliojengeka kwenye biashara nyingi huwa ni matokeo ya tabia za mwanzilishi wa biashara, huwa siyo kitu ambacho kimetengenezwa kwa makusudi ambacho kinaweza kuwa na msaada kwenye biashara hiyo.

Hivyo unakuta biashara imejijengea tabia ambazo siyo nzuri na zinakuwa kikwazo kwa maendeleo ya biashara hiyo. Ukiangalia tabia za biashara hiyo, zinakuwa zinaendana sana na tabia za mwanzilishi wa biashara hiyo.

breakthrough

Mfano kama mwanzilishi wa biashara ni mzito kwenye kufanya maamuzi, basi ufanyaji wa maamuzi wa kila mtu kwenye biashara unakuwa ni mzito sana. Maamuzi hayafanyiki kwa wakati na biashara inazikosa fursa nzuri za kukua zaidi.

Kama mwanzilishi wa biashara hawezi kupangilia vitu vyake vizuri kwenye maisha yake binafsi, unakuta biashara nayo haina mpangilio mzuri, vitu vipo hovyo hovyo na hakuna utaratibu wowote unaotumika kwenye kufanya vitu.

Kama mwanzilishi wa biashara ana tamaa, biashara nzima inaendeshwa kwa tamaa, kila aliyepo kwenye biashara hiyo anakuwa na tamaa na kujali mambo yake zaidi kiliko ya biashara.

Hivyo popote ambapo biashara imekwama, kwa hakika ndipo ambapo mmiliki wa biashara hiyo amekwama. Biashara haiwezi kukua zaidi ya ukuaji wa mmiliki wa biashara hiyo.

SULUHISHO NI MFUMO.

Suluhisho pekee la changamoto hii ya biashara kuwa na tabia zinazoizuia kukua, ambazo zimetoka kwa mwanzilishi wa biashara hiyo ni kuwa na mfumo sahihi wa kuendesha biashara.

Biashara inapoendeshwa kwa mfumo, inakuwa na tabia zake yenyewe ambazo ni bora na haziathiriwi na tabia binafsi za mmiliki wa biashara au mfanyakazi anayefanya kazi kwenye biashara hiyo.

Mfumo unaweka nafasi za kazi na majukumu ambayo mtu anapaswa kuyatekeleza. Lakini pia mfumo unaeleza jinsi ambavyo mtu anapaswa kutekeleza majukumu hayo.

Hivyo mtu yeyote anapokuwa kwenye biashara hiyo, anategemewa kufanya na kuzalisha matokeo ya aina moja, ambayo yanasimamiwa na mfumo.

Rafiki, kama unataka biashara yako isiathiriwe na tabia zako binafsi, kama unataka kuacha kuwa kikwazo kwenye ukuaji wa biashara yako kama ulivyo sasa, suluhisho ni mfumo.

JE UNAWEZAJE KUTENGENEZA MFUMO?

Watu wengi wanaposikia kutengeneza mfumo wa biashara basi hufikiria biashara inabidi iwe kubwa sana, iwe na wakurugenzi, mameneja na ofisi nyingi kwa ajili ya nafasi mbalimbali zinazotengenezwa kwenye mfumo huo.

Lakini hii siyo sahihi, kila biashara, hata ambayo inaendeshwa na mtu mmoja inaweza kuendeshwa kwa mfumo na ikaweza kukua sana.

Tena ukianza biashara kwa mfumo ukiwa peke yako, ni rahisi biashara hiyo kukua kwa sababu unapoanza kuajiri, unawaweka watu moja kwa moja kwenye mfumo badala ya kuwaajiri halafu kujiuliza wafanye nini.

Wengi pia wamekuwa wanafikiria ili kutengeneza mfumo kwenye biashara zao itawagharimu kiasi kikubwa sana cha fedha. Lakini hili siyo kweli pia, unaweza kutengeneza mfumo wako mwenyewe bila ya gharama za ziada.

KARIBU KWENYE SEMINA YA MFUMO WA BIASHARA.

Rafiki yangu mpendwa, kwa kuelewa umuhimu mkubwa wa kuwa na mfumo kwenye biashara zetu, nimekuandalia semina ya MFUMO WA BIASHARA.

Hii ni semina ambayo itakupa maarifa sahihi na hatua za kuchukua ili wewe mwenyewe uweze kutengeneza mfumo kwenye biashara yako na kuiwezesha biashara yako kukua zaidi.

Semina hii itafanyika kwa njia ya mtandao wa wasap hivyo unaweza kushiriki ukiwa sehemu yoyote ile duniani, huku ukiendelea na majukumu yako ya kila siku.

Semina hii itaanza rasmi tarehe 04/07/2019 mpaka tarehe 14/07/2019, kila siku asubuhi utapata somo la semina na utaweza kuuliza maswali kuhusiana na somo hilo. Masomo yote yatatumwa kwenye kundi la wasap na hivyo utaweza kuyafuatilia kwa urahisi.

Japokuwa semina hii inafanyika kwa njia ya mtandao, utajifunza kwa kina sana na kuondoka na mengi ya kwenda kufanyia kazi kuliko unavyoweza kujifunza kwenye semina ya kuhudhuria ana kwa ana. Kwa sababu semina hii ya mtandaoni inakwenda kwa kina sana kitu ambacho siyo rahisi kukifanya kwenye semina ya siku moja ya ana kwa ana.

JINSI YA KUSHIRIKI SEMINA YA MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA.

Rafiki, ili uweze kushiriki semina hii nzuri sana itakayokupa uhuru kamili wa maisha yako, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Semina hii itaendeshwa moja kwa moja kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni moja ya programu za mafunzo na ukocha ninayoendesha, ambapo watu wanajifunza na kuhamasika kila siku, kisha kuchukua hatua na maisha yao kuwa bora sana.

Kama tayari wewe ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ada yako iko hai basi tayari umeshajihakikishia kushiriki semina hii. Wewe jiandae tu, kaa mkao wa kujifunza na utaondoka na nondo za kwenda kuiendesha biashara yako vizuri.

Kama ni mwanachama lakini ada yako inaisha karibuni, lipa ada yako mapema ili usikose nafasi ya kushiriki semina hii. Hakikisha hutoki ndani ya KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kunufaika zaidi na mafunzo haya na mengine mengi.

NJIA MBILI ZA KUSHIRIKI KWA WASIO WANACHAMA WA KISIMA CHA MAARIFA.

Kama wewe siyo mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ungependa kushiriki semina hii ya MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO, kuna njia mbili unazoweza kutumia kushiriki semina hii.

Njia ya kwanza ni kujiunga na kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Hapa unalipa ada ya mwaka ambayo ni tsh laki moja (100,000/=). Kwa kulipa ada hiyo unapata nafasi ya kuwa ndani ya KISIMA CHA MAARIFA kwa mwaka mzima tangu tarehe uliyolipia. Utapata mafunzo ya semina mbili zinazofanyika mtandaoni kwa mwaka, na pia utapata nafasi ya kuwa karibu na mimi kocha wako, tukijifunza kwa kina. Pia tunakwenda kuwa ka Klabu za KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinakupa jumuiya ya watu ulionao karibu ambao wanapiga hatua kufanikiwa zaidi.

Njia ya pili ni kujiunga na kundi maalumu kwa ajili ya semina hii. Kama huwezi kulipa ada ya mwaka ya KISIMA CHA MAARIFA au kama hutaki kuendelea kujifunza kila siku, unaweza kupata masoko ya semina hii kwa kujiunga na kundi maalumu la semina hii. Kundi hili litakuwa hai wakati wa mafunzo ya semina na baada ya semina kuisha litafungwa. Ili kujiunga kwenye kundi hili maalumu, unapaswa kulipa ada ya kushiriki semina pekee, ambayo ni tsh elfu 20 (20,000/=) na hapo utaweza kuyapata masomo haya mazuri na kuiwezesha biashara yako kufanikiwa sana.

Chagua sasa rafiki yangu utashiriki semina hii kwa njia ipi kati ya hizo mbili, kwa kuwa mwanachama au kujiunga na kundi maalumu. Wito wangu kwako ni usikubali kutokushiriki semina hii, ni kosa ambalo hutajisamehe kwenye maisha yako.

Kwa wale ambao wamechagua kushiriki kwa kundi maalumu, bonyeza kiungo ninachoweka hapa ili kujiunga na kundi maalumu la semina. Kiungo ni hiki; https://chat.whatsapp.com/LRtdAqkeDD0BgJXzzoPR6t kama tayari umeshakuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA usijiunge na kundi hilo maalumu. Hilo ni kundi kwa wale wanaotaka kushiriki semina pekee na siyo wanachama.

JINSI YA KULIPA ADA.

Ili kulipa ada ya kushiriki semina hii, tuma kwenye namba zifuatazo;

TIGO PESA / AIRTEL MONEY – 0717 396 253 (Jina AMANI MAKIRITA)

M-PESA – 0755 953 887 (Jina AMANI MAKIRITA)

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa wasap  kwenda namba 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia SEMINA YA MFUMO WA BIASHARA.

MWISHO WA KULIPIA ILI KUSHIRIKI SEMINA.

Rafiki, mwisho wa kulipia ada yako ya KISIMA CHA MAARIFA au KUNDI MAALUMU ili uweze kupata mafunzo ya semina hii ni tarehe 01/07/2019.

Ili ujihakikishie kushiriki semina hii na kuweza kuikuza biashara yako, lipa ada yako mapema kabla ya tarehe hiyo ya mwisho.

Ninaamini unapenda sana kupiga hatua na kufanikiwa kwenye biashara yako,

Ninaamini hilo linawezekana kabisa, kwa sababu nimeona wengi wakianzia chini na kupiga hatua zaidi.

Na nina imani kubwa kwenye mafunzo niliyokuandalia, yanakwenda kukupa uhuru mkubwa sana kwenye maisha yako, hata kama biashara yako ni ndogo sana.

Karibu sana ushiriki semina hii ya MFUMO WA BIASHARA na utaweza kupiga hatua zaidi. Kama siyo mwanachama basi bonyeza kiuongo hiki ujiunge na kundi maalumu la semina hii; https://chat.whatsapp.com/LRtdAqkeDD0BgJXzzoPR6t

Na kumbuka kulipa ada yako kwa wakati, kabla ya tarehe 01/07/2019 ili uweze kunufaika na mafunzo haya yatakayoiwezesha biashara yako kukua zaidi.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge