Katika safari yako ya maisha ya mafanikio, mara zote kazana kukaa upande wa ukweli.

Kwa sababu ukweli huwa hauna huruma.

Wote tunajua ya kwamba ukweli una umiza. Na wengi tunapenda kutafuta njia za kuondokana na maumivu ya ukweli.

Lakini mara zote ukweli huwa hauachi kuwa ukweli, unaendelea kuwa ukweli bila ya kujali wewe unapenda au hupendi.

Dunia inatoa nafasi nyingi za watu kuukimbia ukweli, lakini ukweli huwa hauna haraka, unabaki kuwa ukweli na kuna siku yule anayeukimbia ukweli atakutana nao ana kwa ana na ataumia sana.

Kwa kila unachofanya, kaa upande wa ukweli.

Ni bora kuukabili ukweli mapema na ukaumia, kuliko kuukwepa na ukaja kuukabili baadaye, kwa sababu utakapoukabili ukweli baadaye utakutana na maumivu makubwa zaidi.

Ione dunia kama ilivyo, na siyo kuiona kama unavyotaka kuiona wewe. Kuiona dunia kama ilivyo kutakuumiza, lakini siyo kama maumivu utakayoyapata kwa kujidanganya na baadaye kuja kukutana na ukweli.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha