“To what service is my soul committed? Constantly ask yourself this and thoroughly examine yourself by seeing how you relate to that part called the ruling principle. Whose soul do I have now? Do I have that of a child, a youth . . . a tyrant, a pet, or a wild animal?”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 5.11
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ambayo tumeiona leo.
Ni bahati ya kipekee kwetu kuiona siku hii, kwani siyo kila aliyepanga kuiona ameweza kuiona.
Hivyo basi ni wajibu wetu kutumia nafasi hii ya leo vizuri, kwa kufanya yale yaliyo sahihi kulingana na vipaumbele vyetu.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari MAENDELEO YA NAFSI…
Ni wajibu wa kila mmoja wetu kupima maendeleo ya nafsi yake,
Kwa sababu maendeleo ya nafsi ndiyo yanapima mafanikio kwenye maisha.
Katika kupima maendeleo ya nafsi yako, jiulize ni kitu gani ambacho umejitoa kufanyia kazi, wapi ambapo unataka kufika.
Ukishajua majibu hayo, angalia zile hatua unazochukua kila siku, je zinakupeleka kule unakotaka kufika?
Watu wengi wamekuwa wanapotelea njiani kwa sababu hawajihoji na kujitathmini kwenye kila hatua wanayopiga.
Hivyo wanakuwa na malengo na mipango mikubwa, lakini hatua wanazochukia hazihusiani kabisa na malengo waliyonayo.
Anza leo zoezi la kujihoji na kujitathmini maendeleo ya nafsi yako, ili uweze kuona kama hatua unazochukua zinaendana na malengo na mipango uliyonayo.
Kama haviendi sawa basi chukua hatua mara moja.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kufanya yale ambayo yanaendana na malengo na mipango mikubwa uliyonayo ili uweze kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.
#JifanyieTathmini, #FanyaKilichoSahihi, #EndelezaNafsiYako
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1