“My reasoned choice is as indifferent to the reasoned choice of my neighbor, as to his breath and body. However much we’ve been made for cooperation, the ruling reason in each of us is master of its own affairs. If this weren’t the case, the evil in someone else could become my harm, and God didn’t mean for someone else to control my misfortune.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 8.56
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana kwetu.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari JITAWALE MWENYEWE…
Kila mtu anapenda kuww huru, lakini inapokuja kwenye kufanya maamuzi kuhimu sana kwenye maisha, watu huanza kuangalia wengine wanafanya nini au wanasema nini.
Hii ni kuchagua kuwa mtumwa wa wengine, kutawaliwa na watu wengine.
Kama unataka kuwa na uhuru kamili wa maisha yako, basi unapaswa kujitawala wewe mwenyewe.
Unapaswa kufanya maamuzi kwa sababu zako mwenyewe na siyo kwa sababu za wengine.
Unapaswa kuwa tayari kufanya mambo yako na kuwaacha wengine nao wafanye yao.
Siyo rahisi hili, kwa sababu binadamu ni viumbe wa kijamii, huwa tunapenda kuwa sehemu ya jamii, kwa kufanya yale ambayo wengine wanafanya.
Kumbuka hakuna aliyepata mafanikio makubwa kwa kufanya yake ambayo kila mtu anafanya.
Wote waliofanikiwa sana walichagua kuyaishi maishw yao, na kuachana na maisha ya wengine.
Kuna wakati wengine hao waliwaona kama watu waliochanganyikiwa, au wasiojua nini wanataka. Lakini mwisho wa siku waliochagua kuishi maisha yao wanafanikiwa, na waliochagua kuiga maisha ya wengine wanabaki na maisha magumu ya kuigiza.
Chagua kuyaishi maisha yako leo, kwa mipango yako kwenyewe na uhuru mkubwa kabisa. Pia waache wengine nao waishi maisha waliyochagua wao wenyewe.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuchagua kuishi maisha yako, siku ya kujitawala wewe mwenyewe.
#JitawaleMwenyewe #IshiMaishaYako #AchaMaigizo
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1